TAKUKURU MAKETE WAAGIZWA KUCHUNGUZA MIRADI HII SHULE YA SEKONDARI MATAMBA NA SHULE YA MSINGI MANGA
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa Charles kabeho amegoma kuzindua mradi wa Vyoo vya kisasa Shule ya Sekondari Matamba kata ya Matamba Wilayani Makete
Mradi huo umegharimu Milioni 58 ukiwa umejenga vyoo 23 ambavyo Kiongozi wa Mwenge amesema ameridhika na ubora wake lakini gharama zilizotumika amezikataa kuwa hana uhakika kwa kuwa gharama ni kubwa kuliko Matundu ya vyoo ambayo ni machache
Kiongozi huo amesema vyoo hivyo vingejengwa angalau kwa Milioni moja kila tundu angeridhia lakini siyo gharama hizo zilizotumika ambazo ni zaidi ya Milioni 2.5 kwa kila tundu
Mradi huo umefadhiliwa na shirika la SAWA na ameagiza TAKUKURU Wilaya ya Makete kufuatilia uhalali wa manunuzi ya vifaa vilivyotumika na uhalisia wa fedha
Mchana huu amegoma kuzindua mradi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya Walimu Shule ya Msingi Manga ujuni kwa Madai ya mradi kuwa chini ya kiwango
No comments