MAHAFALI YA KIDATO CHA SITA MWAKAVUTA HIGH SCHOOL YAFANA WILAYANI MAKETE MKOANI NJOMBE
Wanafunzi 182 wa Kidato cha sita Mwakavuta High School jana wamefanya Mhafali yao ya kuhitimu masomo baada ya kuwepo shuleni hapo kwa kipindi cha miaka miwili
Haya ni Mahafali ya saba kwa wanafunzi hao kufanyika shuleni hapo tokea kuanzi kwa Kidato cha tano na cha sita shuleni hapo,Mahafali hayo yalifana kwa aina yake ya kipekee
Katika Risala yao kwa Mgeni Rasmi Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ihiho Mh.Jisoni Mbalizi aliyefika shuleni hapo kushiriki Mahafali hayo wamesema shule yao imekuwa ikiweka Historia ya kukumbukwa kila mwaka kulingana na ubora wa Taaluma inayopatikana shuleni hapo
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo LUKA MKAKATU amesema Mahafali hayo yamekuwa ya aina yake huku wakifurahia Matunda yanayopatikana shuleni hapo kwa kuzidi kuongezeka kwa Kiwango cha Taaluma kwa wanafunzi na nidhamu bora
Mgeni rasmi katika Mahafali hayo Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe Ndg.JASERY MWAMWALA aliyewakilishwa na Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ihiho Mh.JISONI MBALIZI ameahidi kutoa mifuko kumi ya Saruji shuleni hapo kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za Ujenzi
Angalia picha zote za Mahafali hayo hapa chini
Wahitimu wa Kidato cha sita wakiwa katika pozi
Wanafunzi wakicheza Sebene na kukabidhiwa zawadi na wanafunzi wenzaoWanafunzi wa kidato cha tano wakipita mbele ya wahitimu na kuonyesha mavazi ya Heshima ya dini ya kiislam
Makamu Mkuu wa Shule ya Mwakavuta High School Mwl.Shukuru Sanga akifurahi jambo wakati akifuatilia matukio mbalimbali kwenye Mahafali hayo
Wanafunzi wa kidato cha tano wakionyesha Mavazi yanayovaliwa na wataalamu wa Masuala ya Afya
Mwanafunzi akiigiza mavazi yaliyokuwa yakibuniwa na wazazi wa kata ya Iniho ili yavaliwe na wanafunzi wakati wa kuanzishwa kwa shule hiyo
Wanafunzi wakiigiza Maisha ya Uzee yalivyo Mtaani
Wageni waalikwa wakisiliza jambo kwa umakini
Mwalimu Mkuu wa shule ya Mwakavuta High School Luka Mkakatu akizungumza kwenye mahafali hayo
Serikali ya Viongozi shuleni hapo(Kutoka kulia ni Maria Sotel Dada mkuu wa shule,kulia kwake ni Paul Kasebele Kaka Mkuu wa shule,anayefatia ni Katibu wa shule Bw.Obitas Tiras,wa pili kushoto ni Emmanuel Mwakasagule Kiongozi wa nidhamu na wa mwisho kushoto ni Steveb Mwakalembe kiongozi wa Mazingira shuleni hapo)
Huyu ni Mzazi kutoka Chimala Mbeya Remmy Joseph Mfaume akitoa naaha zake kwa wanafunzi wote waagwa na waaga kwa niaba ya wazazi
Mlinzi wa shule akisakata Lumba mara baada ya kujumuika na wanafunzi wanaohitimu huleni hapo
Kushoto ni Mkuu wa shule ya Mwakavuta High School Mlw.Luka Mkakatu akitoa Historia ya shule hiyo kwa Mgeni Rasmi,wageni waalikwa na wanafunzi
Wanafunzi wakionyesha vipaji vyao kwa kuruka mchezo wa Sarakasi
No comments