Header Ads

WANANCHI KUTOKA VIJIJI SITA VYA KATA YA MANG'OTO WANATARAJIA KUANZA UJENZI WA BWENI LA WAVULANA BAADA YA MWANAFUNZI KULICHOMA LILILOKUWEPO



Wananchi wa Vijiji vya Kata ya Mang'oto wameanza taratibu za Ujenzi wa Bweni la Wavulana shule ya Sekondari Mang'oto baada ya Bweni lililokuwepo kuchomwa na Mwanafunzi wa Kidato cha pili(15) Mvulana mwanzoni mwa wiki hii tarehe 12 March 2018

Wananchi hao wamekubaliana kila kijiji kuchangia tofali elfu tano,Mawe trip tatu na fedha Shilingi Milioni moja ili kupata kiasi cha Shilingi Milioni sita kutoka vijiji sita vya kata hiyo ya Mang'oto huku Diwani wa kata hiyo Mh.Osmund Idawa akiahidi kuchangia Laki mbili kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kazi hiyo

Vijiji vinavyoshiriki katika ujenzi huo wa Bweni ni Usungilo,Mang'oto,Makangalawe,Ilindiwe,Ibaga na Mlembuli 

Mnamo tarehe 14 March 2018 wananchi na viongozi wa kata na vijiji walikutana na kukubaliana kwamba kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi za Maendeleo achangie elfu kumi na mwisho wa Mchango ni tarehe 10 April 2018

Ujenzi wa Bweni unatarajiwa kuanza mara moja ili kupunguza adha wanayoipata wanafunzi waliounguliwa Vifaa vyao kama nguo,Madaftari,Vitanda,Magodoro na vitu vingine ambapo kwa sasa wanafunzi 142 wanalala kwenye Madarasa 

Baada ya tathmini kufanyika ili kubaini gharama ya Mali zilizoteketea Mkuu wa shule ya Sekondari Mang'oto Bonivetura Pangani amesema ni Zaidi ya shilingi Milioni mia moja na nane laki nane thelathini na moja elfu

No comments

Powered by Blogger.