HOSPITALI YA BULONGWA NA ZAHANATI ZA(KKKT-DKK) ZILIZOPO WILAYANI MAKETE SASA KUWA CHINI YA SERIKALI
Jackob Meena Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete akisaini Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano kati ya Serikali na KKKT-DKK katika kuhudumia Wananchi kwa kutoa huduma bora za Afya Hospitali ya Bulongwa na Zahanati mbalimbali kwenye Hoteli ya Madihani Villa's Makete Mjini
Serikali imeingia Mkataba wa miaka mitatu wa kufanya kazi na Hospitali pamoja na Zahanati zinazomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kusini Kati (KKKT-DKK) Wilayani Makete Mkoani Njombe.
Makubaliano hayo yamefanyika hii leo katika Hotel ya Madihani Villas ambapo Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Makete Ndugu JACOB MEENA amesema kuwa makubaliano hayo yataleta faida kubwa ya ya upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa wananchi waliokuwa wakitembea umbali mrefu kufuata huduma za afya kwenye vituo na Zahanati za Serikali baaada ya kushindwa kupata huduma stahiki kwenye Zahanati nyingi zilizokuwa zinamilikiwa na KKKT-DKK kutokana na baadhi Zahanati na Hospitali ya Bulongwa kukosekana kwa baadhi ya huduma.
Mganga mkuu wa Wilaya ya Makete Daktari Itikija Msuya ameomba ushirikiano mkubwa kati ya Hospitali au Zahanati zilizokuwa zikimilikiwa na Taasisi ya Kidini chini ya DKK Makete na Serikali ili kuboresha upatikanaji wa huduma bora za Afya kwa Wananchi
Kwa upande wake Daktari John Mcheshi Mkurugenzi wa Idara ya Afya Dayosisi ya Kusini kati amesema Mkataba huo utasaidia kutatua changamoto iliyokuwa inazikumba zahanati zilizokuwa chini ya DKK hususani changamoto kubwa iliyokuwepo ya upungufu wa watumishi wa Afya na Hospitali ya Bulongwa
Pia ameongeza kwamba Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli anaimani itasaidia kuongeza watumishi wenye weledi na kazi katika kuboresha Afya kwenye Hospitali ya Bulongwa na Zahanati mbalimbali
Silvester Mathiasi Udope ni Meneja wa Kanda ya kusini tume ya Kikristo ya huduma za jamii (CSSC) amesema kwa Mkoa wa Njombe Mkataba huu ni wa kwanza kufanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Makete na anaamini utakuwa na tija kwa Jamii katika upatikanji wa Huduma za Afya
Katika Wilaya ya Makete Zahanati na Hospitali zilizokuwa zikimilikiwa na (KKKT-DKK) ni Hospitali ya Bulongwa,Zahanati ya Unenamwa,Ihanga,Igolwa,Ugabwa,utengule na utanziwa
No comments