Header Ads

WANANCHI KIJIJI CHA MATAMBA WAGOMEA KUPOKEA TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI UJENZI WA DAHARIA MATAMBA SEKONDARI WILAYANI MAKETE




Wananchi wa kijiji cha Matamba wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika mapema wiki hii kijijini hapo
  Afisa Mtendaji kata ya Matamba Telesia Emmanuel akisoma taarifa ya Mapato na Matumizi ya mchango wa Daharia shule ya Sekondari Matamba mbele ya wananchi waliofika kwenye mkutano huo
Diwani wa kata ya Matamba Mh.Epheli Ng'ondya(CHADEMA) akizungumza na Wananchi wa Matamba
Hansi Makoti aliyekuwa kada wa CCM Kijiji cha Matamba akikabidhiwa kadi ya Chadema baada ya kujiunga na chama hicho kwa madai ya kuridhishwa na majibu aliyoyatoa diwani wake katika mkutano wa hadhara kuhusu ujenzi wa daharia katika shule ya sekondari Matamba

Wananchi wa kijiji cha Matamba kata ya Matamba wilayani makete mkoani Njombe wamekataa kuipokea taarifa ya mapato na matumizi ya ujenzi wa daharia katika shule ya sekondari Matamba iliyopo kijijini hapo

Hayo yameibuka katika mkutano wa diwani wa kata hiyo na wananchi wa kijiji hicho, ambapo wananchi wamehitaji risiti zinazoonesha matumizi ya fedha hizo pamoja na mchanganuo wa kila kijiji kimechanga kiasi gani

Afisa Mtendaji wa kata hiyo Teresia Emmanuel Lameck ndiye aliyesoma taarifa hiyo ya mapato na matumizi kwa wananchi hao na katika maelezo yake wananchi wakagomea kuipokea taarifa hiyo

Hali hiyo ikawafanya wananchi wahoji baadhi ya mambo waliyoona hayakwenda sawa katika taarifa hiyo


Diwani wa kata hiyo Mh Epheli Ng'ondya akaungana na wananchi wake kuagiza maamuzi ya wananchi yafanyiwe kazi, lakini amewaomba wananchi kuendelea na ujenzi wa daharia hiyo hata kama wameikataa taarifa hiyo

Wananchi hao wamekubali kuendelea na ujenzi wa daharia hiyo huku diwani huyo akiwaasa wananchi kuwaepuka viongozi wa kisiasa wanaofika kwenye kata yake na kupiga siasa badala ya kufanya kazi kwani muda wa siasa haupo na kwa sasa ni wakati wa maendeleo

Katika hatua nyingine mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo mwananchi aitwaye Hansi Makoti akakihama chama cha Mapinduzi na kujiunga na chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kwa madai ya kuridhishwa na majibu aliyoyatoa diwani wake katika mkutano wa hadhara kuhusu ujenzi wa daharia katika shule ya sekondari Matamba


Mwanachama huyo akapokelewa na Mwenyekiti wa CHADEMA kata ya Matamba Hashim Nyambo na kukabidhiwa kadi ya CHADEMA na kutakiwa kwenda kuwajibika kama chama hicho kinavyotaka

No comments

Powered by Blogger.