Header Ads

UBOVU WA BARABARA MAKETE BADO NI TATIZO KUBWA

 Hali ya barabara ilivyo
 Picha zilizopigwa na wadau zikionyesha hali ya barabara ilivyo kwa sasa 

Barabara ya Nkenja kuelekea Ujuni kata ya Kitulo kwenda Mbeya

Changamoto ya Barabara katika maeneo mengi Wilayani Makete hususani kipindi hiki cha Mvua za Masika imesababisha kushuka kwa Mapato ya wajasiriamali kufuatia kushindwa kusafirisha Mazao yao kupeleka sokoni

Wananchi wa Tarafa ya Matamba na Ikiwo wamezungumza na Kitulo na kuelezea hali halisi ya Barabara hiyo ambayo inawafanya kuchukua muda wa zaidi ya Masaa sita kufika Chimala Mbeya badala ya muda wa saa moja waliokuwa wakitumia kusafiri kipindi cha Kiangazi

Mariamu Ngogo Mkazi wa Matamba anasema "Ndugu Mwandishi hili siyo tatizo dogo ni kubwa mno hivi unavyotuona hapa tumeondoka saa nane mchana Mbeya lakini sasahivi ni saa mbili bado tupo barabarani na hatujui tutafika saa ngapi nyumbani" aliongea Bi.Mariamu

Bi Mariamu ameongeza kuwa tunaomba Mh.Diwani wa Matamba,Mh.Mbunge waliangalie jambo hili kwa ukaribu zaidi maana hali ni mbaya ya usafiri

Alatunonga Sanga anasema kilio kikubwa cha Wananchi ni tatizo la Barabara 

Kondakta wa Gari la Kampuni ya Mipango ya Mungu Golden Ngogo gari linalofanya safari za Matamba-Chimala-Mbeya amesema changamoto ya barabara ni kubwa na kusababisha kusafiri zaidi ya saa tano kutoka Chimala mpaka Matamba na kuongeza kuwa hiyo imewafanya kufika Matamba usiku sana kutokana na ubovu wa Barabara

Mariamu Said Fundi Sanifu Barabara kutoka ofisi ya wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Wilayani Makete amesema Ofisi hiyo inatambua ubovu wa barabara hiyo na tayari kwa mwaka wa fedha 2017/18 ameshapatikana mkandarasai kwa ajili ya Matengeneo kwenye maeneo korofi Kilomita nne Barabara hiyo ya Matamba-Chimala kulinagana na hali mbaya ya ubovu wa Barabara iliyopo kwa sasa

No comments

Powered by Blogger.