BARABARA YA LAMI CHIMALA-MATAMBA-KITULO IPO KWENYE MCHAKATO
Serikali imesema Ujenzi wa Barabara ya Lami
kutoka Chimala kupitia Matamba mpaka Kitulo ni Muhimu kwa Maendeleo ya nchi na wananchi wa Makete ikiwa ni pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Kitulo iliyopo
Wilayani Makete Mkoani Njombe
Serikali imesema kwa sasa inamchakato wa
kuboresha Barabara zilizomo kwenye hifadhi za Taifa ikiwemo barabara ya
Chimala,Matamba –Kitulo na Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi
Mawasiliano na uchukuzi imesema itaendelea kuona umihimu wa Barabara hiyo kama
Mh.Norman Sigalla King Mbunge wa Jimbo la Makete alivyoomba Barabara hiyo iweze kujengwa kwa Kiwango cha Lami
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri Wizara
ya Maliasili na Utalii Mh.Hasunga Bungeni jijini Dodoma hapo jana wakati akijibu swali la
Mbunge wa Jimbo la Makete Mh.Prof.Norman Sigalla King aliyetaka kujua Je ni lini
Serikali itaanza ujenzi wa Barabara ya Lami kutoka Chimala-Matamba mpaka kitulo
kwa manufaa ya wananchi wa Maeneo hayo na kukuza utalii katika hifadhi ya Taifa
ya Kitulo
thanks kama itakuwa kweli
ReplyDelete