WANAFUNZI MSIKUBALI KURUBUNIWA NA MIATANOMIATANO:MONNY LUVANDA
Naibu Katibu wa Chama cha Maendeleo Makete(MDA) Bi.Monny Luvanda akizungumza na wanafunzi wanaosoma Mang'oto Sekondari
Akizungumza
na wanafunzi pamoja na Vijana waliofika shule ya Sekondari Mang’oto iliyopo
kata ya Mang’oto Wilayani hapa Naibu Katibu wa Chama cha Maendeleo Makete(MDA) Bi.Monny Luvanda ambaye pia ni Mzazi na Mlezi wa watoto amesema inaleta taswira
mbaya kwa Vijana kujiingiza kwenye masuala ya Kimapenzi katika umri wa chini ya
miaka 18 na ukizingatia wengi wao kwa umri huo wanakuwa Mashuleni na sheria
inazuia kujihusisha kimapenzi katika Mazingira hayo
Pia
Bi.Monny Luvanda ameongeza kuwa Mabinti wengi huwa wanarubuniwa na Vijana wa
Mitaani kwa miatano miatano ambazo ni danganyatoto kwani Mambo hayo yanapita na
watakuja kuyaona Mtaani wakati wao ukifika
“Mkipata
Mimba au Ukimwi katika umri huu na mkaanza kuugua nani atapaswa kumuhudumia
mwezie kati ya wewe mtoto na Mzazi? Aliwauliza wanafunzi ambao walimjibu kwa
kusema sisi ndio tegemeo na siyo Mzazi kuanza kumuuguza tena mwanaye”
“Mtoto
unatakiwa ujilinde,usimame katika nafasi yako ili uje kuwa Faraja kubwa kwa
Mzazi wako hapo baadaye,Nawaomba Muangalie kilichowaleta hapa shuleni ni Masomo
tuu”
“Ukiona
mtu anakusumbua kuwa muwazi mwambie hata Mwalimu au mzazi kuwa kuna mtu ananisumbua
ili usije kukatisha masomo yako bure kwa kupewa ujauzito au kuambukizwa
magonjwa,Wanangu,wadogo zangu haya mambo yapo tu na yanapita tafadhali sana
someni kwa bidii”
Bi.Monny
Luvanda alimaliza kusema “Elimu ni Mkombozi wa Maisha yenu na Mungu awabariki
sana niwatakie Amani ya Mungu AMINA”
No comments