SERIKALI IPO MBIONI KULETA PUNDAMILIA HIFADHI YA TAIFA KITULO
Maua yakionekana na mwonekano wa kuvutia katika Hifadi ya Taifa Kitulo
Wananchi
Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuzitumia fursa za kuwekeza katika Hifadhi
ya Taifa ya Kitulo.
JOFREY
WILSONI KYANDO ni moja kati ya Viongozi
kutoka Hifadhi ya Taifa Kitulo amesema ndani ya Hifadhi hiyo kuna fursa za
uwekezaji kwa Wananchi ikiwemo kujenga Nyumba
za kulala wageni pamoja na kujenga sehemu za kupiga mahema kwa ajili ya kulala wageni ndani ya Hifadhi
hiyo.
JOFREY
WILSONI KYANDO amesema ‘‘Fursa kubwa
tuliyonayo katika hifadhi ya kipekee ni kivutio kikubwa ambacho hakipatikani
kwenye hifadhi nyingine yeyote i ni maua lakini tunayo fursa nyingine ya
uwekezaji ni kujenga Hoteli za Kisasa,kujenga Lodge na kujenga sehemu za kupiga
Mahema kwa ajili ya watalii Fursa hizo ziko wazi kwa Watanzania wote na watu
wengine kutoka nje ya Tanzania”
“Kwa
hiyo tunapenda kuchukua fursa hii ya Utalii kwa watu wote bila ubaguzi kwa
ajili ya kukuza uchumi wa Nchi yetu pendwa ya Tanzania”
Bwana
JOFREY amewatoa hofu wanamakete na
Tanzania kuondokana na dhana ya kusema kuwa Hifadhi ya Taifa ya Kitulo haina
wanyama ilihali Hifadhi ina wanyama wadogo wadogo na hivi karibuni hifadhi hiyo
ipo mbioni kuleta wanyama wakubwa wakiwemo pundamilia.
Hifadhi
ya kitulo ni moja kati ya hifadhi kumi na sita Nchini na ni Hifadhi inayosifika
kuwa na kivutio kikubwa na cha kipekee
cha maua ambacho hakipatikani katika
Hifadhi yeyote ile.
Pia
unaweza kufanya utalii wa kutembelea maporomoko ya Maji,kupiga mahema,Utalii wa
picha,kuona wanyama wadogowadogo kama digidigi,swala,nyani,utalii wa kutembea
kwa miguu vitu vingine vingi
Kwa
Mtanzania ni Muhimu sana kutembelea Hifadhi za Taifa ili kujionea maajabu mengi
na yenye kuvutia katika Hifadhi zilizopo hapa Nchini
Hifadhi
ya Taifa ya Kitulo ni Hifadhi ya Taifa la Tanzania iliyopo katika Mkoa wa
Njombe na Mbeya,ambapo awali ilijulikana kama Elton Plateau baada ya Mvumbuzi
Fredrick Elton kupitia eneo hilo mnamo mwaka 1870
Mwaka 1960 Shirika la Chakula na Kilimo (FAO) lilichukua eneo hili kwa ajili ya ukulima wa ngano na ufugaji wa kondoo.
Baadaye likageuzwa kuwa shamba la ng'ombe ambalo lipo hadi leo. Kutokana na umuhimu wa eneo hili wadau mbalimbali wa mazingira walipendekeza eneo hili litangazwe kuwa hifadhi ya taifa ili kulinda umaridadi wa maua na mimea adimu inayopatikana ndani ya eneo hili.
Mwaka 2005, Kitulo ilitangazwa rasmi kuwa hifadhi ya Taifa ikijumuisha sehemu ya eneo la shamba la mifugo, Msitu wa Livingstone na bonde la Numbi kiasi cha kilometa za mraba412.9 ndani ya mwinuko wa mita 2100 na 3000 juu ya UB.
Hifadhi hii inasifika kwa kuwa na maua aina mbalimbali na zaidi ya aina 30 hupatikana Kitulo pekee na maeneo kusini mwa Tanzania.
Pia ndilo eneo pekee Tanzania ambapo ndege aina ya Tandawili machaka (Denhams Bustard) wana makazi. Wapo aina mbalimbali ya ndege kama vile Mpasua mbegu mweusi(Kipengere seed eater) na wengineo.
Jamii mpya ya nyani (Lophocebus Kipunji) waligunduliwa mwaka 2003 Kitulo. Hifadhi hii ina uwanda wa tambarare, mabonde, vilima na maporomoko ya maji. Ndani ya msitu, kuna miti aina ya cidar yenye urefu wa zaidi ya mita 50 na inakadiriwa kuwa mirefu kuliko yote duniani.
Kitulo inafikika kwa gari kutoka Chimala, kilometa 78 mashariki kwa mji wa Mbeya. Pia unaweza kufika ukitokea Zambia kupitia Tunduma au Malawi kupitia Karonga kwa barabara.
Reli ya TAZARA hupita karibu na hifadhi ya Kitulo.
No comments