ASKOFU MTEULE KKKT-DKK MAKETE ATOA PONGEZI KWA CHAMA CHA MAENDELEO MAKETE (MDA)
Askofu
Mteule Dayosisi ya Kusini Kati Wilson Sanga amewataka wanaMakete kushirikiana
katika kuiletea Maendeleo Wilaya ya Makete bila kujali itikadi zao za Kidini huku
akiumwagia sifa Ushirikiano walionao WanaMakete waishio ndani na nje ya Makete
kupitia Chama cha Maendeleo Makete MDA kwa shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Chama hicho katika Wilaya hii
Askofu
Mteule Sanga ameyasema hayo Mapema wiki hii wakati wa Mazungumzo ya Pamoja kati
yake na Viongozi wa Chama cha Maendeleo Makete MDA sambamba na Baraza la
Viongozi wa Dayosisi hiyo ya KKKT DKK Makao Makuu ya Dayosisi hiyo Makete Mjini
Mkoani Njombe
Askofu
Mteule Wilson Sanga amesema kupitia Chama cha Maendeleo Makete (MDA) na
WanaMakete Mbalimbali waliyoungana kupitia Mitandao ya Kijamii kama Makundi ya
WatsApp wamejiunga katika kusaidia shughuli mbalimbali za Maendeleo Makete na
kwenye Dayosisi hiyo ili kuangalia namna bora ya kuboresha Huduma mbalimbali
zinazotolewa na Dayosisi hiyo Kielimu,Kiafya na hata Kidini katika Kuibua na
kuendeleza Miradi inayosimamiwa na Dayosisi hiyo
Wakati huo
huo Askofu Mteule ameipongeza MDA kwa Mchango mkubwa walioutoa Shule ya
Sekondari Mang’oto kwa kutoa vifaa mbalimbali vya ujenzi wa Bweni la Wavulana
na kuongeza kwamba Kanisa pia linamchango wake mkubwa katika shule ya Sekondari
Mang’oto hivyo kwa kufanya hivyo wamelisaidia Kanisa pia
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Maendeleo Makete MDA Wakili Philipo Mahenge akizungumza
na Askofu huyo Mteule,Msaidizi wa Askofu pamoja na Baraza la Uongozi wa
Dayosisi hiyo amesema nia ya MDA ni kuongeza ushirikiano baina ya Chama hicho
na Taasisi Mbalimbali zikiwemo za Kidini katika Kuiletea Maendeleo Wilaya ya
Makete
Pia
amewapongeza waumini wa Dini hiyo ya Kikristo kwa Uchaguzi uliofanyika katika
kumpata Baba Askofu Mteule Wilson Sanga
Kwa upande
wake Msaidizi wa Askofu Mch.Adili Pagalo amewapongeza WanaMakete kwa kuungana
kupitia Chama cha Maendeleo Makete MDA kwa shughuli mbalimbali wanazozifanya
ambazo ni za Kimaendeleo kwa Wilaya ya Makete,huku akiwataka WanaMakete waishio
Nje ya Makete kuwa na kumbukumbu ya kurudi kwao na kuwekeza kwenye Miradi ya
Maendeleo ili kuikuza Makete Kiuchumi
Award
Mpandila ni Katibu wa Chama cha Maendeleo Makete (MDA) amesema MDA siyo Chama
cha Kisiasa na MDA imeamua kushirikiana na Taasisi mbalimbali zikiwemo za
Kidini hivyo Chama kinajipanga kuhakikisha kinawaunganisha WanaMakete katika
kuleta Maendeleo Makete kupitia ushirikiano kutoka kwa Wadau Mbalimbali wa
Maendeleo
Na katika
Sherehe zinazotarajiwa kufanyika mwezi ujao za kumuweka wakfu Askofu Mteule
Mdau wa Maendeleo Makete Bw.Award Mpandilah ameahidi kuchangia
kiasi cha shilingi Laki moja kwa ajili ya kusaidia Maandalizi ya
sherehe hiyo ya kuwekwa wakfu kwa Baba Askofu
Kutoka kushoto ni Katibu wa MDA Award Mpandila,akifuatiwa na Askofu Mteule Wilson Sanga,Katikati ni Naibu Katibu wa MDA Bi.Monny Luvanda,wapili kulia ni Wakili Philipo Mahenge na wa kwanza Kulia ni Msaidizi wa Askofu KKKT-DKK Mch.Adili Pagalo
Askofu Mteule KKKT-DKK Wilson Sanga Kulia akisoma Katiba ya Chama cha Maendeleo Makete(MDA) baada ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa MDA Philipo Mahenge
Askofu Mteule KKKT-DKK Wilson Sanga kushoto akisikiliza jambo kutoka kwa Viongozi wa MDA hawapo pichani akiwa na Baraza lake
Award Mpandila akizungumza wakati wa Mazungumzo ya Pamoja kati ya Viongozi wa Chama cha Maendeleo Makete MDA sambamba na Baraza la Viongozi wa Dayosisi hiyo ya KKKT DKK Makao Makuu ya Dayosisi hiyo Makete Mjini
No comments