MTOTO ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUDUMBUKIZWA KWENYE SHIMO LA CHOO MAKETE-NJOMBE
Mtoto wa umri wa miaka (13)
anusurika kifo baada ya kutumbukizwa kwenye shimo la choo lenye urefu wa mita
24,kuokoa uhai wa mnyama (mbuzi) kwa ujira wa Tsh.1000/=(elfu moja ) na soda
moja tukio lililotokea hivi karini katika kijiji cha bulongwa kilichopo kata ya
bulongwa wilayani makete mkoani njombe .
Akizungumza na waandishi wa
habari Mwenyekiti wa kitongoji cha lupaso bw,VELEHIM NAHOLI SANGA,amekili
kutokea kwa tukio hilo kwenye kitongoji chake huku akitoa onyo kwa
wananchi kuondokana na vitendo vya
kikatili dhidi ya watoto.
Wakiwa kwenye mkutano wa
kitongoji cha Lupaso baadhi ya wanchi wa
kijiji cha bulongwa wamasema tukio hilo
limetokea siku ya Jumamosi mnamo tarehe 25/11/2017 majira ya mchana ambapo Bi,
Huruma John Mahenge alifanya tukio hilo la kikatili dhidi ya mtoto mwenye umri wa
miaka (13) anaye soma darasa la tano (5) katika shule ya msingi Bulongwa lakumshawaishi na kumtumia motto huyo kuokoa uhai wa mbuzi
aliye tumbukia kwenye choo kinachotumika kwa kumfunga kamba aina aya manira kiunoni
mtoto huyo jamabo ambalo nikinyume cha sheria ya mtoto no 21 ya mwaka 2009.
Twingitsiwe Mahenge ni bibi mlezi
wa mtoto amesema mtoto huyo alifanyiwa kitendo hicho siku ya jumamosi ambapo
yeye siku hiyo hakuwepo nyumbani na mara baada ya kurudi alibaini kudhoofu kwa mtoto
huyo jambo lililompelekea kumuuliza na
kubaini kuwa mjukuu wake amefanyiwa ukatili hivyo alichukue hatua ya kutoa
taarifa kwa viongozi wa kitongoji ili kupata msaada zaidi
Kwaupande wa mtoto
aliyefanyiwa ukatili amesimlia jinsi alivofanyiwa kitendo hicho huku akieleza
jinsi tendo hilo lilivyo muathili kiafya na kwamba alilazimishwa kufanya tukio
hilo na alipo jaribu kukataa alitishiwa kuwa chapwa na shangazi yake ambaye
nimhusika wa tukio hilo.
Waandishi wa habari
walipofanya mahojiano na mhusika watukio hilo aliyetambulika kwajina la HURUMA JOHN MAHENGE amekili kufanya tukio
hilo huku akieleza kuwa alifanya kitendo hicho pasipo kujua kama ni kosa kwa muujibu wa sheri na baadaya kugundua kuwa
nikosa aliwaomba radhi ndugu huku akilili kumpekeka mtoto hospitari kwaajili ya
vipimo ambapo daktari wazam alimpokea pasipo PF3 na kumpa dawa za maumivu na za
mafua tu
Afisa mtendaji wakata ya
bulongwa bw, YUSTI KONGA, ametoa wito
kwa jamii kutambua utu na thamani ya binadama kwa kutofanya ukatili dhidi ya
watoto kwakuwa watoto wana stili kupata
haki zao za msingi kama binadam wengine pia amesema hatua na sheria itafuata
mkondo wake ili iwefundisho na wawengine.
Bi,mary Mnubi niafia ustawi wa jamii ngazi ya (w) ambaye amesema wamepokea taarifa hiyo ingawa amesema
taratibu za kufuatilia tukio hilo zina endelea na endapo zitakamilika hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi ya mhusika huku akisem vitendo vyakikatili dhidi
ya mtoto havikubliki katika jamii
Kamanda wa pilisi (W) ya
makete OCD – OPTATUSI MAGANGA amekili
kupokea taarifa hizo nakusema kwamba
uchunguzi wa tukio hilo unaendelea
na hatua za kisheria zitachukuliwa ili kuwa fundisho kwajamii nzima.
Juhudi za kumpata daktari
aliye mfanyia uchunguzi mototo huyo bado zinaendelea.
No comments