Msichana abakwa kwa zamu...Mbakaji adai alikuwa akimtamani kwa muda mrefu
KIBARUA
aliyeshtakiwa kwa ubakaji wa zamu Jumatano alisukumiwa kifungo cha
miaka 15 bila faini. Alfred Otieno Oriwo atanyolewa bila maji kwa miaka
hiyo 15 baada ya mahakama kusema “hafai kuishi na wapenda amani.”
Hakimu
mkuu katika mahakama ya Milimani nchini Kenya Francis Andayi alisema
mshtakiwa alimtendea unyama msichana huyo mwenye umri wa miaka 16
aliyemvizia akitoka kununua bidhaa dukani.
Kiongozi
wa mashtaka Bw Solomon Naulikha alimweleza hakimu kwamba mshtakiwa
alikutana na mlalamishi kisha akamshika na kumpeleka katika jengo ambalo
halikuwa limekamilika kujengwa na kumbaka kwa zamu akiwa na wavulana
wengine.
“Lazima
wenye tabia kama yako wajue kuna sheria inayowalinda wasichana na
wanawake kwa jumla. Hupaswi kumtia kumbaka msichana au mwanamke,”
alisema Bw Andayi.
Hakimu alitupilia mbali ushahidi wa mshtakiwa kwamba alikuwa na uhasama na jamii ya mlalamishi ndipo wakamwelekea.
“Ushahidi
uliowasilishwa ulithibitisha wewe ulimbaka mlalamishi baada ya
kumweleza umekuwa ukimtamani kwa muda mrefu,” alisema Bw Andayi.
Mshtakiwa aliamriwa awe akifanyakazi ngumu gerezani ndipo iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama yake.
No comments