Header Ads

WALIMU MWANZA WASEMA TUTAANDAMANA MPAKA KWA MAGUFULI

Walimu mkoani Mwanza wamesema iwapo mkurugenzi wa halmashauri hatawalipa pesa zao za uhamisho, wataandamana mpaka kwa Waziri Mkuu au kwa Rais, ili kupeleka malalamiko yao.


Akizungumza mbele ya waandishi wa habari mmoja wa walimu walioandamana mkoani Mwanza kudai stahiki zao za uhamisho, Mwl. Anicet Majira wa shule ya sekondari Njolay, amesema iwapo hawatalipwa haki zao watalazimika kuendeleza maandamano hayo, licha ya usumbufu mkubwa wanaopata.

“Msimamo wetu ni mmoja, kama leo Rasi alivyolega lega na Mkuu wa Mkoa akashindwa kulitatua hili, moja kwa moja tutakwenda kwa waziri husika, kama waziri husika atashindwa tutakwenda kwa Waziri Mkuu mpaka kwa Rais, kwa hiyo msiamamo wetu ni sisi kulipwa kilicho chetu”, amesema Mwalimu huyo.

Kwa upande wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela, amewataka walimu hao kuwa na subira mpaka tarehe 24 May, ili walitafutie suluhu jambo lao.

Walimu mkoani Mwanza wamendamana leo hii hadi ofisi za Mkuu wa Mkoa ili kudai pesa zao uhamisho, kama serikali inavyotaka

No comments

Powered by Blogger.