MAPAO YAANZISHA KLABU ZA WASAIDIZI WA KISHERIA MASHULENI
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iwawa ambao ni wanachama wa Klabu ya Wasaidizi wa Kisheria wakiwa katika picha ya Pamoja na Walimu walezi,Mkurugenzi wa MAPAO na Mjumbe wa Bodi ya MAPAO
Shirika la Wasaidizi wa Kisheria Wilayani
Makete (MAPAO)limeanza kutoa Elimu ya Kisheria kwa Wanafunzi Shule za Sekondari na Msingi na
kuunda Klabu za Wasaidizi wa Kisheria kwa Wanafunzi hao
Akizungumza na Kitulo Fm Mkurugenzi Mtendaji Shirika hilo Wilaya ya Makete Denis Sinene amesema kuanzishwa kwa
Klabu za Wasaidizi wa Kisheria kwa Shule za Sekondari na Msingi ni Mpango
endelevu kwa ajili ya kutoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kwa shule zote za Sekondari na Msingi
zilizopo Wilayani hapa na nje ya Wilaya
"Kwa sasa tayari tumeanza mchakato wa kufungua Klabu za Wasaidizi wa Kisheria kwenye shule zetu za Sekondari na Msingi na kwa kuanzia tumeanza Iwawa Sekondari ambayo inawanafunzi Zaidi ya mia saba na siyo kwamba wote wapo kwenye Klabu hiyo bali wachache kama hamsini hivi ndio wapo kwenye Klabu hiyo na hao watakuwa Mabalozi kwa wengine kwa kutoa Elimu ya Msaada wa Kisheria kupitia Vipindi mbalimbali na Sanaa"Alisema Mkurugenzi huyo Denis Sinene
"Pia siku chache zijazo tutafungua Klabu nyingine kwa Shule yoyote ya Msingi kutoka kata ya Lupalilo au Isapulano kwenye Shule yoyote itakayoteuliwa"Aliongeza Sinene
Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa uanzishwaji wa Klabu hizo unalenga kuimarisha uelewa wa Wanafunzi kuhusu Sheria Mbalimbali zinazowahusu na Wanafunzi hao watakuwa Mabalozi wazuri kwa Wazazi/walezi wao ambao wanauhitaji na Msaada wa Kisheria watakuja kwa wingi zaidi MAPAO ili kupata Msaada wa Kisheria
Pia ameongeza kuwa uanzishwaji wa Klabu hizo
Mashuleni utaleta unafuu kwa wanafunzi kutambua Sheria ambazo zitaweza
kuwasaidia Shuleni na katika Maisha yao ya hapo baadaye na wengine huenda wakatimiza ndoto zao za kuwa Wanasheria hapo baadaye
Mkurugenzi huyo amesema kwa sasa Elimu ya Msaada wa Kisheria itaendelea kutolewa kwa Wanafunzi shule zote za Sekondari na Msingi ili kuwajengea uwezo wanafunzi wa kutambua Haki zao na Sheria kwa ujumla wake
Walimu walezi wa Klabu ya Wanafunzi wasaidizi wa Kisheria Iwawa Sekondari
Wanafunzi Viongozi wa Klabu hiyo ya wasaidizi wa Kisheria Iwawa Sekondari
No comments