TRA IMEWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUWA MFANO
Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imewataka Watumishi wa Idara za Serikali nchini kuwa mfano katika dhana ya ukusanyaji mapato ya serikali kwa kudai risiti wanapofanya manunuzi ya bidhaa au huduma yoyote wanayolipia.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Festo Kiswaga alipozungumza na Wakuu wa Idara na Watumishi wa serikali mkoani Simiyu katika semina ya matumizi ya Mashine za Kieletroniki za kutoa Risiti za (EFD) iliyoandaliwa na (TRA) ikiwa ni mwendelezo wa kampeni ya mkoa kwa mkoa kutoa elimu na usajili wa walipakodi mkoani Simiyu.
Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA Richard Kayombo alisema Mamlaka hiyo inafarijika sana kupata ushirikiano mzuri toka kwa viongozi na watumishi wa serikali kwa kuunga mkono juhudi za kuhakikisha kuwa serikali inakusanya mapato ambayo yanarudi kuihudumia jamii kwa kuwapatia huduma bora za jamii.
Aidha Meneja wa TRA Mkoa wa Simiyu Charles Mkumbwa alisema semina hiyo ina umuhimu mkubwa kwa watumishi wa umma wanaohusika na malipo mbalimbali.
No comments