SHIRIKA LA MAPAO LAENDELEA KUWAFIKIA WANAFUNZI KWA KUWAPA ELIMU YA MSAADA WA KISHERIA WILAYANI MAKETE
Wanafunzi
Shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kata ya Isapulano Wilayani Makete Mkoani Njombe wameanza
kunufaika na Elimu ya wasaidizi wa Kisheria inayotolewa na Shirika la Makete
Paralegal Organisation(MAPAO)
Mandhari ya Shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kijijini hapo kata ya Isapulano Wilayani Makete yenye wanafunzi 134 kuanzia Darasa la kwanza mpaka Darasa la sita
Mkurugenzi
wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema
utoaji wa Elimu hiyo kwa Wanafunzi ni katika kuwasaidia watoto kuwa na Misingi
bora ya Elimu na kujua haki zao za Msingi ikiwa ni pamoja na wao kutambua
wajibu wao
Mkurugenzi
wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE Ametoa
Maelezo hayo wakati wa kuanzisha Klabu ya Wasaidizi wa Kisheria Shuleni hapo ikiwa ni
Mwendelezo wa kuanzisha Klabu hizo kwenye Shule za Sekondari na Msingi Wilayani
hapa
Akizungumza
na wanafunzi hao Denisi Sinene amesema “Tunafanya kazi za kuisaidia jamii ya
wanaMakete ikiwa ni pamoja na wazazi wenu,ndugu zetu ikiwa ni pamoja na ninyi
watoto mnapokuwa na Matatizo kwenye masuala madogomadogo ya kisheria”
“Jukumu
letu tunaelekeza,tunashauri,tunapatanisha,tunaonya,tunatetea haki za walemavu,tunafundisha
sheria na haki za watoto,wazee na wanawake kwenye kata zote ndio kazi
tunazozifanya”Aliongeza Sinene
Mkurugenzi
huyo ameelezea dhamira na Lengo la kuwepo kwa Wasaidizi wa Kisheria Wilayani
hapa pamoja na kuwataka watoto kuwa watiifu kwa wazazi wao na Jamii
inayowazunguka
Denis
Sinene amesema “Dhamira ya MAPAO ni kuwa na Jamii inayotambua haki za Binadamu
na ninyi ni miongoni mwa Jamii,sasa tunataka jamii hii ijue haki,kwa hiyo
sasa Makusudi ya MAPAO inataka Jamii ijue haki na ninyi pia mjue haki
mbalimbali za Binadamu nanyi muwe na uelewa kuhusu haki zenu”
Kwa
Upande wake Mjumbe wa Bodi ya MAPAO Ndg.Nahumu Tweve amesema wanafunzi hao
wakiendelea kupatiwa Elimu hiyo mara kwa mara Taifa litakuja kuwa na Vijana
waadilifu na kuyaishi mema wakati wote
Nahumu
Tweve amesema “Wapo wahalifu ndio maana
ipo Sheria sasa ninyi mkilelewa katika Misingi yenye Maadili naamini mtakuwa
wazalendo,waadilifu,wenye unyoofu na baadaye tutakuwa na Taifa lenye watu
waelewa sasa ninyi shule ya Msingi Luvulunge tunategemea mtakuwa mfano mzuri
kwa watoto kutoka shule zingine ndani na nje ya Wilaya ya Makete kwa kuwa na
watoto waadilifu,wanaojua sheria na wajibu wao”
“Tunategemea
hamtasumbua walimu,hamtasumbua wazazi,hamtalisumbua Taifa kwa sababu mtakuwa
mmeshaelewa wajibu wenu katika Jamii na hapa shuleni mtayaishi yale
tutakayokuwa tunawafundisha,na nyie mkawe mnawafundisha wengine huko nyumbani”
Mkurugenzi
wa Shirika hilo la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete DENIS SINENE amesema
watoto wanatakiwa kujitambua kwa kujua wajibu wao kwa wazazi huku Klabu ya
wasaidizi wa Kisheria iliyoundwa hii leo shuleni hapo ikiwa na wajumbe(Wanafunzi) Zaidi ya
40
Shirika
la Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete MAPAO limeanzisha Klabu 2 za
Wasaidizi wa Kisheria kwa Wanafunzi,Klabu moja kutoka shule ya Sekondari Iwawa kata ya Iwawa na
Klabu nyingine imeanzishwa leo shule ya Msingi Luvulunge iliyopo kata ya Isapulano na hii ni katika Mpango
endelevu wa kutoa Elimu ya Kisheria kwa wanafunzi shule zote za Msingi na
Sekondari Wilayani hapa
Picha mbalimbali kuhusu kilichofanyika leo Shuleni hapo Tazama hapa chini
Wanafunzi wa shule ya Msingi Luvulunge wakisiliza kwa Umakini Elimu iliyokuwa ikitolewa na Viongozi wa MAPAOKutoka kulia ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luvulunge Frolida Ilomo akitambulisha wageni kutoka Shirika la MAPAO waliotembelea shuleni hapo na kutoa Elimu ya wasaidizi wa Kisheria
Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete Denis Sinene akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luvulunge
Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria Wilaya ya Makete Denis Sinene akiimba wimbo wa MAPAO pamoja na wanafunzi wa shule ya Msingi Luvulunge
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa MAPAO Denis Sinene,katikati ni Mjumbe wa Bodi ya Mapao akizungumza na wanafunzi shuleni hapo
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi MAPAO Frolida Ilomo akizungumza jambo
Huu ni ubao wa Mahudhurio ya wanafunzi shule ya Msingi Luvulunge kwa wiki hii
No comments