WANANCHI 39,759 WILAYANI MAKETE WAMEJITOKEZA KWENYE ZOEZI LA UANDIKISHAJI VITAMBULISHO VYA TAIFA(NIDA)
Jumla ya wananchi 39,759 waliosajiliwa na mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA)
Wilayani Makete Mkoani Njombe Kati ya
wananchi 46,317 waliotegemewa
kusajiliwa na vitambulisho vya Taifa NIDA,
Wametakiwa kuwa na subira kwa kuwa kazi ya utengenezaji wa vitambulisho
hivyo inaendelea katika ngazi ya Taifa.
Mratibu wa zoezi la vitambulisho vya Uraia
Kwa Wilaya ya Makete Mwalimu ORGENI
ASHERI SANGA amesema zoezi hilo limekamilika na ufanisi wa zoezi ni kwa
asilimia 85.8
Pia Mwl.ORGENI SANGA amesema zoezi la
usajili wa Vitambulisho vya Taifa (NIDA) litarudiwa kwenye Makao Makuu ya Kata
kwa Wananchi ambao hawajajisajili na
amewataka Wananchi ambao bado hawajajisajili kujitokeza kwa wingi pindi zoezi hizo litakapotanagzwa kuendelea katika Vituo vitakavyokuwa kwenye kata zao
Mwalimu ORGENI SANGA Ameeleza kuwa kwa sasa zoezi hilo kwa limesitishwa kwa muda zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa (NIDA) Kwani
mfumo na computer ambazo wanatumia kusajili umefungwa na jamii imetakiwa
kusubiri wakati utakapofika na kujitokeza kwa wingi Kujisajili.
Mratibu wa Zoezi hilo Wilaya ya Makete Mwl.Orgen Sanga
No comments