WANAFUNZI WANAOSOMA SHULE BINAFSI KUENDELEA KULIPA ADA
Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema wanafunzi wanaosoma katika shule binafasi wataendelea kutozwa ada ya mitihani ya taifa kwa kuwa programu ya elimu bila malipo haizihusu shule hizo hivyo wazazi na walezi ni jukumu lao kugharamia huduma hizo.
Kauli hiyo
imetolewa jana Mei 15, 2018 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
William Ole Nasha Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 29 mkutano wa 11 wa
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu la Mbunge Viti
Maalum Ester Mahawe aliyetaka kujua ni lini Serikali itafuta ada ya mitihani ya
Taifa kwa shule za msingi na sekondari kwa wanafunzi wanaosoma katika shule
binafsi.
Katika
hatua nyingine Serikali imekanusha kuhusu tuhuma za elimu bure kuwa ni ya
kibaguzi kwa wanafunzi nchini hasa kwa wale wanaosoma kwenye shule za binafsi
na kusema kuwa yote wanayofanya ikiwepo kutotoa mikopo kwa wanafunzi wote ni
kutokana na ufinyu wa bajeti.
Pamoja na mambo
mengine Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, William Ole Nasha amesema
serikali itaendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu nchini kadri uwezo wa
kifedha utakaporuhusu kufanya hivyo.
No comments