TAASISI TATU ZAUNGANA KUISHAURI SERIKALI TATIZO LA MAFUTA YA KULA
Wakati jana Rais John Magufuli amefanya ziara ya kushtukiza bandarini na kukagua matanki ya mafuta ya kula na kusema kuwa mafuta hayo yanafaa kwa matumizi ya binadamu, Taasisi tatu zimeungana na kutoa ushauri kwa serikali baada ya mafuta hayo kuadimika mitaani ili tatizo hilo lisijirudie tena.
Taasisi hizo ni Chama Cha Wasindikaji Mafuta ya Alizeti, (TASUPA), Chama Cha Wakulima Wa Alizeti (SUFA) na Taasisi Ya Kumtetea Mlaji Tanzania (TCAS).
"Tupo hapa kwa ajili ya kuzungumzia hii ishu ya uhaba na kupanda kwa bei ya mafuta ya kula tunataka kutoa maoni kwa kile kinachoendelea na kutoa ushauri kwa serikali ili hili suala lisijirudie tena"
"Kwa vyovyote vile suala hili linawaathiri zaidi Watanzania wa kipato cha chini ambao wanategemea bidhaa hiyo kwenye matumizi ya kila siku na kwa wafanyabiashara wa vyakula kunawalazimu kutumia gharama kubwa zaidi kwenye matumizi yao ya kila siku" Ringo Iringo, Mwenyekiti Chama Cha Wasindikaji Mafuta Ya Alizeti Tanzania.
Kuboresha utaratibu au usimamizi wa pamoja miongoni mwa sekta ya umma na binafsi.
Mpango mkakati wa jumuishi wa miaka 5 kwa maendeleo ya sekta ya mafuta ya kula nchini.
Kuboresha huduma ugani.
Kuboresha huduma za kifedha na mitaji kwa wadau- wawekezaji katika viwanda.
No comments