BANK YA NMB YAKABIDHI BATI ZA MILIONI 5 ISAPULANO SEKONDARI.
Bank ya NMB imekabidhi bati 156 zenye thamani ya shilingi Milioni 5 shule ya Sekondari Isapulano Wilayani Makete iliyoanzishwa rasmi mwaka huu na inawafunzi wa kidato cha kwanza tu.
Meneja wa Bank hiyo nyanda za juu kusini Bw.Straton Chilongola akiwa katika makabidhiano hayo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy,M/kiti wa Halmashauri ya Wilaya Mh.Egnatio Mtawa pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya Wilaya,Tarafa,kata na kijiji amesema mchango huo umetolewa kwa lengo la kuunga mkono jitihada zinazofanywa na WanaMakete katika kuboresha Elimu pamoja na kurudisha fadhila kwa wateja wa Bank hiyo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya makete MH.VERONICA KESSY amewataka wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Makete kuendelea kujitoa kusaidia shughuli za maendeleo ili kuiendeleza wilaya ya makete hususani katika sekta ya afya na elimu kama ambavyo baadhi ya wadau wamekuwa wakifanya bila kusahau Chama cha Maendelea Makete ambacho kimekuwa mfano mzuri sana kwenye upande wa Elimu.
Mh.VERONICA KESSY ameongeza kuwa pamoja na jitihada kubwa zinazo fanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dk.JOHN MAGUFULI kuwaletea Maendeleo Wanamakete ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Barabara ya Lami ambayo Mkandarasi yupo kazini hivi sasa kutoka Njombe hadi Makete pamoja na miradi mingine ya kimaendeleo ikiwemo ya Maji,Afya na Elimu lakini bado kunahitajika nguvu ya wananchi wenyewe na wadau wa Maendeleo ili kuijenga Makete kwani Maendeleo huletwa na wananchi wenyewe wa eneo husika.
Naye Meneje wa Taasisis ya fedha ya NMB kanda ya kusini STRATON CHILONGOLA akikabidhi bati hizo kwa Wananchi wa Kata ya Isapulano mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Makete amesema wao kama Taasisi inayo wahudumia Wananchi katika suala zima la fedha wanao wajibu wa kurejesha kile wanacho kipata kwa wananchi ili kuunga mkono shughuli zinazo fanywa na serikali hususani katika sekta ya Elimu,na Afya pamoja na majanga ya muda kama ajali nakuwa Taasisi inayo ongoza kwa kutoa huduma za kifedha kwa wananchi walio wengi nchini.

Mh.EGNATIO MTAWA ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete ametoa pongezi kwa Wananchi wa Kata ya Isapulano waliojitokeza kupokea bati hizo 156 kutoka bank ya NMB kwa michango na nguvu zao walizokuwa wakizitoa toka mwanzo hadi hivi sasa katika ujenzi wa Shule ya Sekondari Isapulano.
Mkuu wa shule ya Sekondari Isapulano Mwl.METHODI SANGA ameishukuru NMB kwa kuwapa bati hizo na kusema hii imekuwa faraja kwao na kuwataka Wananchi wa Kata ya Isapulano kuendelea kujitolea nguvu zao ili kuendeleza ujenzi wa Shule hiyo.
MKUU WA WILAYA YA MAKETE MH VERONIKA KESSY AKIMSHUKURU MENEJA WA NMB BANK KANDA YA KUSINI NDUGU STRATON CHILONGOLA.
WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ISAPULANO WAKIPOKEA BATI PAMOJA VIONGOZI MBALIMBALI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE WAKIFURAHIA KUPOKEA BATI HIZO 156.
MENEJA WA NMB KANDA YA KUSINI NDUGU STRATON CHILONGOLA AKITOA TAARIFA YA BATI HIZO 156.
No comments