CHAMA CHA MAENDELEO MAKETE(MDA) KITAIJENGA MAKETE MPYA
Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy
amwaga pongezi nyingi kwa wadau wa Maendeleo Wilayani Makete kwa Umoja wao na
Ushirikiano walionao katika kuijenga Wilaya yao ya Makete
Pongezi hizo zimetolewa mapema hapo jana
wakati wa Makabidhiano ya Vifaa mbalimbali vilivyotolewa na Wadau wa Chama cha
Maendeleo Makete (MDA) kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Bweni la Wavulana shule
ya Sekondari Mang’oto lililoteketea kwa moto usiku wa tarehe 12 March 2018 na
kutekeleteza vitu mbalimbali vilivyokuwa na thamani ya zaidi ya shilingi
Milioni tisini pamoja na Bweni
Mh.Veronica Kessy amesema “sambamba na Kauli
mbiu ya Chama hicho ya Pamoja tuijenge
Makete kwa ushirikiano huu lazima Makete itajengeka haswa”
“Nimekuwa nikiona harakati Mnazozifanya (MDA)
kwa Umoja wenu najua ninyi ni wawakilishi tu wa wengi waliopo kwenye Umoja huo
lakini sina budi kutoa pongezi zangu za dhati kwa moyo mlionao wa kujitoa kwa
hali na mali katika kuhakikisha mnarudi kwenu na kuwekeza,Mungu yuko pamoja
nanyi na ninaimani kuwa mtawekeza kweli kweli”
“Pia kwa sababu nyinyi MDA mmenifanyia
surprise na mimi nawafanyia surprise vilevile Hili Jengo linalojengwa kwa ajili
ya Bweni la wavulana likikamilika litapewa jina la MDA”
“Sasahivi tunafursa ya ujenzi wa Barabara ya
kiwango cha Lami kutoka Njombe-Makete nadhani mmeona wakandarasi
wanavyochakalika kwa hiyo Makete itafunguka na kuwa kisiwa cha ukuzaji wa
Uchumi siyo Makete tu hata katika Mkoa wetu wa Njombe,kwa hiyo waambieni na
wengine waje waanze kuwekeza Makete hususani katika upande wa Kilimo cha
Matunda Mbalimbali kama Parachichi,apple na Matunda mbalimbali,Mazao ya Viazi
na mazao mengine mengi ambayo kwa ardhi ya Makete aliyoijalia Mungu Neema ya
kila zao kustawi hii ni Fursa kubwa sana kwetu wanaMakete na wana MDA popote
mlipo nasema karibuni sana”Aliongeza Mkuu huyo wa Wilaya
Makamu Mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge
akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Makete vifaa hivyo katika taarifa yake amesema
“Mh.Mkuu wetu wa Wilaya Vifaa hivi ni kutokana na Michango ya wadau mbalimbali
ambao ni wazawa wa Makete na ambao siyo wanaMakete lakini wenye Mapenzi mema na
Makete wameamua kuchanga fedha na kununua vifaa vifuatavyo:-Mifuko 100 ya
Saruji,Bati 150 na Misumari ya bati Kilo 10 kwa lengo la kuhakikisha watoto
wetu,wadogo zetu wanapata mahala pazuri pa kulala ili waweze kusoma katika
Mazingira ya kuvutia”
“Pamoja na jitihada hizi sisi kama MDA
tunatoa pole kwa wote walioathirika na Janga hili la moto,MDA inalengo la
kuwaunganisha wanaMakete waishio ndani ya Wilaya na Nje ya Wilaya katika Nyanja
mbalimbali Kiuchumi na MDA siyo chama cha kisiasa”Aliongeza Ndg.Philipo Mahenge
Philipo Mahenge aliongeza kuwa “Katika Umoja
wetu tuliamua kukusanya Michango mbalimbali kutoka kwa wadau na tumepata
mwitikio mkubwa na waliochangia ni kutoka kwa wadau wenyewe,Makampuni
Mbalimbali yanayomilikiwa na wanaMakete na Kampuni moja ya Kihindi imetuchangia
pia,wanafunzi wenye asili ya Makete wanaosoma vyuo vikuu wamejikusanya na
kuchangia baada ya hapo michango yao wakaiwasilisha kwenye umoja huu na wadau
wengine wasio wanaMakete wenye Mapenzi mema na Wilaya ya Makete”
“Mh.Mkuu wa Wilaya tunawapongeza wananchi
wote wa kata ya Mang’oto na Wilaya yote kwa ujumla kwa hatua muhimu ambazo
mmezichukua katika kuwasaidia wanafunzi ambao wamepatwa na janga la
moto,tunawapongeza pia kwa hatua ya Ujenzi ambayo inaendelea na sisi kama MDA
tunaongeza nguvu na kuwapa ushirikiano pale mlipofikia na ikiwezekana
ushirikiano mwingine utaendelea kuwepo huko mbeleni Hongereni sana”Aliongeza
Unaweza kutizama picha Mbalimbali za tukio
hilo hapa chini
Kutoka kushoto ni Naibu katibu wa Chama cha Maendeleo Makete(MDA) Monny Luvanda,Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge,Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy na wa Mwisho kulia ni Mkuu wa shule ya Sekondari Mang’oto Bonavetura Mgaya ambaye anaelezea hatua ambayo imefikiwa sasa katika ujenzi wa Bweni hilo
Hili ni Jengo linalojendelea kujengwa ambalo
limefikia hatua ya Lenta kwa muda wa wiki mbili
Katika Picha ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy mwenye koti jeusi akiwa na Viongozi wa MDA na viongozi kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Makete
Picha ni Ujenzi wa Bweni ukiendelea na huo ni mwonekano wake kwa mbele
Mkuu wa shule ya Sekondari Mang’oto
Bonavetura Mgaya akielezea Jambo kuhusu shule hiyo ya Sekondari Mang’oto na
kuongeza kuwa kwa sasa wanafunzi zaidi ya mia moja bado wanalala kwenye vyumba
vya Madarasa
Viongozi wa Cahama cha Maendeleo Makete(MDA)
kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge,katikati ni
Katibu wa Chama hicho Bw.Award Mpandila na kushoto kwake ni Naibu Katibu wa
Chama hicho Bi.Monny Luvanda wakiwa kwenye Makabidhiano ya Vifaa hivyo na
kusikiliza taarifa ya Maendeleo ya Ujenzi wa Bweni hilo na mahali ulipofikia
iliyokuwa ikisomwa na Afisa Mtendaji kata ya Mang’oto Bw.Mengi Chalamila
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mang’oto waliofika
shuleni hapo kuhudhuria makabidhiano ya vifaa hivyo
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mang’oto
wakiwasikiliza wageni waliofika shuleni hapo kukabidhi vifaa hivyo
Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Makete
Mwl.Jacob Meena akitoa neon la shukrani kwa wana MDA kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya
Wilaya ya Makete
Bi.Monny Luvanda Naibu Katibu wa MDA akitoa
Salamu za wanaMDA katika Mkusanyiko wa watu mbalimbali waliokuwepo shuleni hapo
Katibu wa MDA Bw.Award Mpandila akitolea
Maelezo namna ya kujiunga na MDA ili uwe Mwanachama na Mkononi akiwa ameshika
Katiba ya Chama hicho ambayo baadaye alimkabidhi Mkuu wa Shule ya Mang’oto
Sekondari ili naye aisome
Award Mpandila akimkabidhi Mkuu wa Shule ya
Sekondari Katiba ya Chama hicho (MDA)
Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge
akizungumza na wananchi wa Kata ya Mang’oto pamoja na wageni mbalimbali
waliohudhuria katika makanidhiano ya Vifaa hivyo
Afisa Mtendaji kata ya Mang’oto Bw.Mengi
Chalamila akisoma taarifa ya Hali ya ukusanyaji wa Michango ilipofikia na hali
ya ujenzi wa Bweni hilo unavyoendelea
Ndg.Burton Sinene kutoka Ofisi ya Mkurugenzi
Wilaya Idara ya Mipango akiwa kama Mjumbe wa Kamati ya Maafa akifafanua jambo
Award Mpandila Katibu wa MDA akiwapa pole
wanafunzi waliounguliwa vifaa vyao vya shule ikiwa ni pamoja na nguo zao katika
Ajali ya moto iliyotokea mwezi March mwaka huu
Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge
akimkabidhi Majina ya waliochangia vifaa hivyo Mkuu wa Wilaya ya Makete
Mh.Veronica Kessy
Award Mpandila Katibu wa MDA akimkabidhi
Majina ya waliochangia vifaa hivyo Mkuu wa Shule ya Sekondari Mang’oto
Mwl.Bonavetura Mgaya
Nembo ya Chama cha Maendeleo Makete yenye
Kauli mbiu ya “Pamoja,tuijenge Makete
yetu”
Makamu mwenyekiti wa MDA Ndg.Philipo Mahenge akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy vifaa vilivyonunuliwa na WanaMDA
Diwani Kata ya Mang’oto Mh. Osmundi Idawa akitoa
neno lake la Shukrani kwa niaba ya ya wananchi kwa wote walioshiriki michango
yao kupitia MDA
Wananchi wa Kijiji cha Makangalawe wakiimba
wimbo wa Shukrani uliokuwa na ujumbe wa kushukuru kwa kile kilichotolewa na
wanaMakete kupitia MDA
No comments