KIJANA WA MIAKA 24 AJINYONGA MPAKA KUFA MSITUNI KIJIJI CHA IVALALILA WILAYANI MAKETE
Kijana Jastini Ilomo (24) mkazi wa kijiji cha Ivalalila kata ya Iwawa Wilayani Makete amejinyonga mpaka kufa kwa kutumia Kamba akiwa kwenye shamba lake la miti ya mbao
Kijana huyo inasadikika alipotea nyumbani tokea jumapili usiku wa kuamkia Jana jumatatu na alikuwa akiishi peke yake baada ya kuachana na mkewe siku chache zilizopita
Haijajulikana sababu ya kujinyonya kwake kutokana na kutokuwepo viashiria vyovyote vya yeye kuamua kuchukua maamuzi hayo,Mwili wake umegundulika hapo jana na kina mama waliokuwa wakisomba mbao msituni takribani kilomita 3 kutoka kijijini hapo
Mwenyekiti
wa Kitongoji cha Kikusi Emmanuel Ilomo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na
kuongeza kwamba Marehemu alipotea katika mazingira yasiyoeleweka siku ya
Jumapili usiku au jumatau asubuhi na jana Jumanne ndipo wakagundua kuwa
amenjinyonga Msituni
Wananachi
wa kijiji hicho akiwemo Baba Mkubwa wa Marehemu wameelezea masikitiko yao
kufuatia tukio hilo huku wakitoa wito kwa wananchi kutochukua maamuzi
yanayoweza kuhatarisha uhai wao badala yake watafute mbadala wa kutatua tatizo
Kaka
wa Marehemu Nickolaus Ilomo anasema Mdogo wake hakuwa na tatizo lolote lakini hajui ni nini
kilichomtokea Mdogo wake mpaka kuchukua maamuzi hayo
Mwili wa Marehemu umezikwa jana,MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI ALIPOPACHAGUA ENZI ZA UHAI WAKE AMINA.
No comments