Header Ads

TMA YAWATAKA WANANCHI KUCHUKUA TAHADHARI

Mamlaka ya hali ya hewa iliyopo chini ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewatahadharisha wananchi kuwepo kwa vipindi vya mvua kubwa na upepo mkali unaozidi km 50 na zaidi kwa saa katika maeneo yote ya pwani kuanzia saa 24 zijazo kutoka sasa.
Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mamlaka hiyo jioni ya leo (Jumatatu) na kudai kutakuwepo vipindi vya mvua kubwa katika saa 24 ambavyo vinatarajiwa katika maeneo ya mkoa wa Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba.
Mbali na hilo, TMA imesema kuna tarajiwa maeneo ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini yanatarajiwa kuendelea kupata vipindi vifupi vya mvua kubwa na hali ya mawingu huku Maeneo mengine ya nchi yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi.
Kwa taarifa kamili angalia hapa chini..

No comments

Powered by Blogger.