Header Ads

NJOMBE:CHF ILIYOBORESHWA KUWAFIKIA WANANCHI SASA HUDUMA ZA MATIBABU NI NDANI YA MKOA

Kufuatia Maboresho ya Mfuko wa Afya ya Jamii CHF kwa wananchi ,wananchi Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuanza kujiandaa ili siku chache zijazo wajiunge kwa wingi zaidi katika mfuko huo ili waweze kupata huduma za Afya kwa gharama nafuu na bei ndogo


Kwa sasa Serikali imefanya maboresho hayo kutoka shilingi Elfu kumi kwa kaya yenye Jumla ya watu watano mpaka kufikia watu sita kwa kaya na malipo ya shilingi Elfu Thelathini na huduma hiyo itapatikana kwa mwaka Mzima kwenye Kituo chochote cha Afya au Hospitali yoyote ya Serikali

Rai hiyo imetolewa na Mganga Mkuu Wilaya ya Makete Dkt.Itikija Msuya katika mafunzo ya siku tatu yaliyoanza kutolewa hapo jana kwa Waganga wafawidhi,Hospitali,Vituo vya Afya na Zahanati zinazomilikiwa na Serikali kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete

Ameongeza kwamba Huduma hiyo pindi itakapoanza kutolewa Mwanachama ataweza kutibiwa popote ndani ya Mkoa wake kwenye kituo cha kutolea huduma za Afya kinachomilikiwa na Serikali

Clemence Ngajilo kutoka Ipelele Mshiriki wa Mafunzo hayo na Mwenyekiti wa Bodi ya Afya Wilaya amesema mfumo huu unaokuja kwa sasa anaona umelenga kuwasaidia wananchi wengi waliokatika hali ya chini kimkaisha katika kupata huduma za Matibabu kwa gharama nafuu kwenye Mkoa husika

Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt.John Magufuli imesema ina nia ya dhati kuboresha huduma za Afaya kwa Watanzania wote bila kujali hali zao kiuchumi na kijamii

No comments

Powered by Blogger.