KATIBU MKUU (UWT)TAIFA AMINA NASSORO MAKILAGI AMWAGA MISAADA KWA WAGONJWA KITUO CHA AFYA MATAMBA NA WATOTO YATIMA WILAYANI MAKETE
Katibu wa Umoja wa Wanawake chama cha Mapinduzi (UWT)Taifa Mh.AMINA NASSORO MAKILAGI alipowatembelea akinamama wajawazito Kituo cha Afya Matamba
Katibu wa Umoja wa Wanawake chama cha Mapinduzi (UWT)Taifa Mh.AMINA NASSORO MAKILAGI akiwa katika picha ya Pamoja na watoto Yatima wanaoishi kituo cha kulelea watoto Yatima FEMA MATAMBA
Katibu wa Umoja wa Wanawake chama cha Mapinduzi (UWT)Taifa Mh.AMINA NASSORO MAKILAGI akigawa vitu mbalimbali kama Sabuni kwa wagonjwa waliolazwa kituo cha Afya Matamba Wilayani Makete
Katibu wa Umoja wa Wanawake chama cha Mapinduzi (UWT)Taifa Mh.AMINA NASSORO MAKILAGI amehaidi kutoa mashuka na vitanda 2 vyenye thamani ya Shilingi Milioni mbili Kituo cha Afya Matamba Wilayani Makete Mkoani Njombe kwa ajili ya kutumika kwenye wodi la akinamama Wajawazito.
AMINA NASORO MAKILAGI ametoa ahadi hiyo akiwa kwenye ziara yake ya siku 2 Wilayani Makete Mkoani Njombe kwa lengo la kukagua miradi mbalimbali iliyopo chini ya Serikali ambayo inatekelezwa kupitia Ilani ya Chama cha Mapindizi
Akiwa katika Ziara hiyo Wilayani hapa amekagua kituo cha Afya Matamba,pia ametoa sabuni za kipande katoni 5 na sabuni ya unga pakti 20 kwa wagojwa waliolazwa kituo cha Afya Matamba.
BRAITONI NDANDALA ni Mkuu wa kituo cha Afya Matamba amemshukuru Katibu wa UWT Taifa kwa kutembelea kituo hicho na kutoa misaada hiyo huku akiongeza kwamba Kituoni hapo kunaupungufu mkubwa wa wahudumu na vyumba vya kufanyia upasuaji kwa akina mama wajawazito kwani kituo cha Afya Matamba kinapokea na kuhudumia wagojwa wengi wajawazito wanaohitaji huduma ya upasuaji
Amesema kituo hicho kwa mwezi kinapokea na kuhudumia wagonjwa wasiopungua Themanini jambo ambalo linakumbana na Changamoto kubwa ya upungufu wa Chumba cha upasuaji na Wahudumu wa Afya
Wakati huohuo Katibu wa UWT amejitolea kuwa mlezi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha FEMA kilichopo Kata ya Matamba kinacho milikiwa na Baba Askofu ALA MBWILO na ametoa katoni 4 za sabuni na sabuni ya unga pakti 20 na katoni 1 ya biskuti na akisema kuwa atakuwa mlezi msaidizi wa kituo hicho cha fema Matamba kwani amefurahishwa na kazi kubwa inayofanywa na Askofu Mbwilo.
Akisoma historia ya kituo hicho mbele ya Katibu wa UWT Taifa mama Askofu Mbwilo amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2010 kikiwa na Lengo kuwasaidia watoto yatima kutoka kata mbalimbali zilizopo Wilayani Makete Mkoani Njombe.
AMINA MAKILAGI amewataka watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha FEMA kuwa na heshima kwa watu wanaowalea na kuwaheshimu watu wote
Kituo cha FEMA Matamba kwa sasa kinajumla ya watoto Yatima 12 ambao wapo katika ngazi mbalimbali za Elimu ya Msingi
No comments