WANAFUNZI WATORO KUSWEKWA RUMANDE WILAYANI MAKETE
Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ihiho Mh.Jisoni Mbalizi akizungumza kwenye Mahafali ya kidato cha sita Mwakavuta sekondari yaliyofanyika jana shuleni hapo
Wanafunzi watoro shuleni na wasiohudhuria Vipindi vya Masomo Darasani Wilayani Makete Mkoani Njombe kusekwa Rumande
Agizo hilo limetolewa hapo jana na Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete ambaye pia ni Diwani wa kata ya Ihiho Mh.Jisoni Mbalizi Mgeni rasmi kwa niaba ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe Jasery Mwamwala akiwa katika Mahafali ya Kidato cha sita Mwakavuta Sekondari iliyopo Kata ya Iniho Wilayani hapa
Mh.Jisoni Mbalizi amemuagiza Afisa Mtendaji kata ya Iniho kuwakamata na kuwaweka ndani wanafunzi wote watoro na wanaokimbia vipindi vya Masomo ili iwe fundisho kwa wengine kuacha tabia hiyo mbaya na kuinua kiwango cha taaluma Wilayani Makete
''Wengi hususani wavulana huwa wanazurula sana huko mtaani wanakunywa pombe na ulanzi kama watu wazima na familia zao wakati ni wanafunzi,sasa nakuagiza Mtendaji wa kata Kamata wote weka ndani wajifunze''
''Na kama kuna wanafunzi wanatumia simu ole wao wakamatwe na kama wapo waache mara moja''ameongeza Mbalizi
Katika Hatua nyingine Mh.Jisoni Mbalizi amesema kitendo cha Mwanafunzi kujihusisha kimapenzi ni kosa kisheria na hii husababisha wanafunzi kupata Mimba na Magonjwa baadaye kushindwa kutimiza Malengo yao kimaisha
Ameongeza kuwa Janga la Ukimwi bado ni kubwa kwa Wilaya ya Makete na kuwataka wanafunzi kutojihusisha na Mapenzi kwa kuwa ni hatari kwao na kutoendekeza ngono zembe ili kutimiza Malengo yao
Wakati huohuo amewataka Wazazi kuwa Makini na watoto wao pindi watakapokuwa wanarudi Majumbani kwao kwa kuwalinda wasije kuwaachia wajukuu na wao kuishia kuugua magonjwa na kubeba mizigo ya Malezi
No comments