WANAUME WATAKIWA KUWA WAVUMILIVU KWA WAKE ZAO
Wanawake kwa Wanaume Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuwahi Hospitali mara wanapoona
dalili za hatari kwa mama Mjamzito ili kupatiwa matibabu.
ROSEMERY LUVANDA ni muuguzi Hospitali ya Wilaya ya
Makete Kitengo cha Mama na Mtoto amesema kuwa Wanaume na wanawake wanapoona
dalili za hatari kwa mama mjamzito wanatakiwa kuwahi kufika katika kituo chochote cha kutolea
huduma za Afya ili kupata elimu juu ya dalili za awali zinavyotokea kwa mama Mjamzito.
BI.ROSEMERY ameiomba Jamii ya Wanamakete kutambua dalili za
hatari anazoweza kuzipata mama Mjamzito ikiwa ni pamoja na maumivu ya kichwa,
kuumwa kwa tumbo chini ya kitovu,pamoja na kujisikia kizunguzungu ambacho
husababishwa upungufu wa damu.
ALAMOKA MAHENGE ni mama Mjamzito kutoka Kijiji cha Iwawa Mamlaka ya Mjimdogo wa Iwawa amewataka wanaume kuwajibika kuwasindikiza wake zao Klinic mara wanapoona mwanamke ni mjamzito ili kupata
elimu juu ya dalili za hatari kwa mama mjamzito na amewataka wanaume kuwa na uvumilivu
pindi mama anapokuwa mjamzito .
No comments