SHULE YA MSINGI YENYE VYUMBA VINNE VYA MADARASA NA WANAFUNZI KUANZIA DARASA LA KWANZA MPAKA LA SABA WILAYANI MAKETE HII HAPA
Shule
ya Msingi Imehe iliyopo Kata ya Bulongwa ni miongoni mwa shule kongwe Wilayani
Makete lakini bado inakabiliwa na uhaba mkubwa wa kutokuwa na vyumba vya
Madarasa na kusababisha kufanya vibaya kwenye Matokeo ya Darasa la nne na la
saba kila mwaka
Shule
ya Msingi Imehe inajumla ya wanafunzi 137 kuanzia Darasa la kwanza mpaka Darasa
la saba na inavyumba vinne tu vya Madarasa na inajumla ya walimu wanne
wanaofundisha shuleni hapo,shule hiyo ilianzishwa mwaka 1976 ikiwa na jumla ya
wanafunzi 30
Tokea
kuanzishwa kwa shule hiyo imekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu
wa vyumba vya Madarasa hali inayopelekea wanafunzi kusoma kwa mlundikano jambo
ambalo linaweza kusababisha wanafunzi kuugua magonjwa mbalimbali hususani ya
kuambukiza na kusababisha kuwa na matokeo mabaya kwa wanafunzi
Kwa
upande wa taaluma shule hiyo bado imekuwa na changamoto kubwa ya ufaulu duni
kulingana na wanafunzi kushindwa kusoma katika Mazingira rafiki badala yake
darasa moja linatumiwa na Madarasa mawili kwa wakati mmoja pamoja na baadhi ya
wanafunzi kutembea umbali mrefu kulingana na Jiografia ya kijiji hicho kuwa na
Milima mingi
Shule
ya Msingi Imehe kwa sasa inauhitaji wa vyumba vitano vya Madarasa ili kukidhi
idadi ya Wanafunzi na vyumba vya kusomea pamoja na kuwa na ofisi ya walimu
Mpango
uliopo hivi sasa katika kukabiliana na hali hiyo ni kupata vyumba viwili vya
Madarasa pamoja na ofisi moja ya walimu vyenye thamani ya shilingi Milioni 50
mchango unaotarajiwa kuombwa/kukusanywa kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo
wazawa wa kijiji cha Imehe waishio ndani ya nje ya kijiji hicho,Taasisi
mbalimbali,Serikali pamoja na nguvu za wananchi wenyewe
Wananchi,Wazaledo
na wadau wa Maendeleo na wapenda Elimu Wilayani Makete mnaombwa kusaidia katika
ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya Madarasa ili kunusuru hali iliyopo katika
shule hiyo kwa kupunguza mlundikano wa wanafunzi Darasani na kuongeza ufaulu
kwa wanafunzi wa shule hiyo ya Msingi Imehe
Mwonekano wa Majengo ya shule ya Msingi Imehe
Hiki ni chumba kinachotumika kama Darasa lakini pia kinatumika kama stoo ya shule hiyo
Mwonekano wa chumba kimojawapo kwa ndani kinachotumika kuwafunzia wanafunzi wa shule ya Msingi ImeheMandhari ya kijiji cha Imehe
No comments