NAMNA AMBAVYO MARIA NA CONSO WALIVYOFARIKI KWA MPISHANO WA DAKIKA KATI YA 10 NA 15
Mganga
mfawidhi Hospitali ya Rufaa Iringa Museleta Nyakiroto ameeleza namna ambavyo safari ya Maria na
Consolata ilivyokuwa “Mnamo tarehe 17 May 2018 majira ya saa moja nusu jioni
wakiwa wametokea Hospitali ya Taifa Muhimbili walikokuwa wakipatiwa Matibabu
baada ya kuruhusiwa lakini waendelea kupata Matibabu wakiwa nyumbani”
“Rufaa ya
iringa tulitakiwa kuendelea kufanya ufatiliaji kwa Maria na Conso wakiwa nyumbani,kwa hiyo
walifikishwa Iringa na Ambulance na walisindikizwa na Daktari,Muuguzi mmoja na
Technical mmoja wa Mambo ya ICU kwa ajili ya ile mitungi ya gesi ambayo
wamesafiri nayo, kwa hiyo lengo lao na letu ilikuwa ni kuwapumzisha ili
wakipumzika basi waruhusiwe kwenda
nyumbani”
“Kwa hiyo
tangu hiyo tarehe 17 May tumekuwa tukiwahudumia hapa rufaa Iringa wakiendelea kupata
matibabu mbalimbali ikiwemo Oxygen kwa hiyo tangu siku hiyo hatukuona kama
wanapata unafuu sasa mpaka jana ilipofika majira kati ya saa 2:30 mpaka saa 3
usiku wakawa wamefariki”
“Aliyenza
kufariki ni Maria baadaye Consolata naye akawa amefariki walipishana dakika kumi
mpaka kumi na tano hivi”
No comments