Header Ads

MAGUFULI ATEUA MWINGINE

Katika kuhakikisha adhima yake ya kesi kumalizika kwa wakati na haki kupatikana inatimia, Rais Magufuli ameendelea kuboresha utendaji kazi wa Mahakama Kuu nchini kwa kumteua Mhe. Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania.

Rais Magufuli amefanya uteuzu huo Juni 2, 2018 na Jaji huyo pamoja na wengine walioteuliwa hivi karibuni wanatarajia kuapishwa Juni, 4, 2018 Ikulu jijini Dar es salaam

Rais mara nyingi amekuwa akisisitiza juu ya kesi kushughulikiwa kwa wakati ikiwemo zile zinazohusu masuala ya rushwa pamoja na migogoro mbalimbali ikiwemo ya ardhi pamoja na miradi ya maendeleo.

Taarifa ya Ikulu hapo chini inaeleza kwa undani zaidi.

No comments

Powered by Blogger.