MBUNGE JIMBO LA MAKETE PROF.NORMAN SIGALLA KING AMEKABIDHI SHILINGI LAKI TANO NA BATI 50 UKARABATI WA MADARASA S/M TANDALA
Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.NORMANI SIGALLA
KING ametoa bati Hamsini pamoja na kiasi cha fedha Taslimu shilingi laki Tano na
nusu ilikusaidia ukarabati wa jengo moja
katika shule ya Mazoezi Tandala iliyopo Kata ya Tandala Wilayani Makete Mkoani Njombe
Akikabidhi bati hizo hii leo kwa niaba ya
Mbunge Katibu wa Mbunge FELIX KYANDO amesema Mbunge wa Jimbo la Makete ameamua kuongeza nguvu za wananchi wa Tandala kwenye ukarabati wa chumba kimojawapo cha Darasa shule ya Msingi Tandala kwa ajili ya kuhakikisha wanafunzi wanapata Elimu katika Mazingira rafiki kwa watoto
Pia Ndg.Felix Kyando ameongeza kuwa Mh.Mbunge ni mpenda
maendeleo na yuko tayari kuunga mkono nguvu za wananchi katika shughuli za
maendeleo hivyo Wananchi wa Makete watambue kwamba mwenye nacho huongezewa ni vema na wao pia wakatoa nguvu zao kwenye
suala zima la Maendeleo
Pia Mh.Mbunge mapema mwaka huu alikabidhi kiasi cha shilingi laki tano na nusu shuleni hapo kwa ajili ya ukarabati wa majengo shuleni hapo
Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Tandala Simoni
Haule amemshukuru Mh.Mbunge wa Jimbo la Makete Prof.Normani Sigalla King kwa kujitolea kwake
katika kuunga mkono jitihada zinazo fanywa na wananchi wa Kata ya Tandala katika
ukarabati wa jengo hilo
Mwl.Simoni Haule ameongeza kuwa wanatarajia kuezua paa la jengo lenye vyumba vitano vya Madarasa shuleni hapo ambalo linavuja hususani kipindi cha Masika na kulazimika kufanyia ukarabati wa kiwango cha juu sambamba na Ofisi moja ya walimu
No comments