MWENGE WA UHURU KUZINDUA MIRADI 9 WILAYANI MAKETE
Wananchi Wilayani Makete Mkoani Njombe wametakiwa kuupokea
mwenge wa uhuru kwa shangwe katika maeneo ambayo mwenge huo utapita kuanzia eneo la
mapokezi, maeneo ya uzinduzi wa Miradi na Matukio Mbalimbali ambayo
mwenge wa uhuru utapita.
Hayo yamesemwa na mratibu wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Makete BRUNO MWANGWALE ambaye amesema wanananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi katika
maeneo ambayo Mwenge wa Uhuru utapita.
BWANA BRUNO MWAGWALE amesema Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 utapokelewa Tarehe 30 May 2018 kata ya mfumbi ukitokea wilaya ya Wanging'ombe na utakagua miradi 9 iliyopo katika Kata ya Matamba,Kitulo,Iwawa,Lupalilo na Tandala
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa vyoo bora
matamba ,Klabu ya kupambana na Rushwa Matamba ,Vyumba vya Madarasa na Nyumba ya Mtumishi Lupalilo kijiji cha Ugabwa pamoja na kukagua shughuli za kimaendeleo ambazo zinafanya na
wanafunzi wa chuo cha Veta makete
Wakati huohuo Mwenge wa Uhuru utatembelea Ofisi za Halmashari ya wilaya ya Makete na kutembelea Ofisi za Redio Kitulo kwa kutambua kazi ambazo zinafanywa na Kituo hiki cha Redio ambapo utakesha Stendi ya Tandala kata ya Tandala Wilayani hapa
Pia Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru atasoma
ujumbe wa mbio za mwenge moja kwa moja (live) kupitia redio Kitulo Fm.
No comments