AFARIKI DUNIA KWA KUKANYAGWA NA GARI KIJIJI CHA IWAWA WILAYANI MAKETE
Mtu mmoja
aliyetambulika kwa jina la Aleso Mahenge(41) mkazi wa Iwawa amefariki Dunia kwa
ajali ya kukanyagwa na Gari aina ya Isuzu Truck T597 AUW mwishoni mwa wiki
iliyopita
Ajali hiyo
ilitokea mnamo tarehe 15 May 2018 saa 6 mchana kijiji cha Iwawa mtaa wa
Dombwela akiwa kazini wakati wa kutengeneza kwenye Gereji ya Kumbuka Mahenge Wilayani
Makete Mkoani Njombe
Mashuhuda wa
Ajali hiyo wamesema Marehemu Aleso Mahenge alikuwa na wenzake wakisukuma gari
hiyo lakini kwa bahati mbaya ikiwa na Dereva ndani yake iliserereka kwa nyuma
na kumgonga Aleso ambaye alikanyagwa kwenye Mguu na kusbabisha Kupoteza uhai
wake
Chrisantus
Kavishe Kaimu Mkuu wa Polisi Wilaya ya Makete ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi
Wilaya ameeleza kuwa Chanzo ya ajali hiyo ni Dereva kukosa Umakini wa kulimudu
gari
Dereva huyo
aliyetambulika kwa jina la Orgeni Mtenzi (42) mkazi wa Iwawa Wilayani hapa amekamatwa na atafikishwa
Mahakamani pindi ushahidi utakapokamilika na Jeshi la polisi linaendelea na
uchunguzi kuhusu tukio hilo
No comments