"TUNATAKIWA KUWAOMBEA VIONGOZI WETU" MH.BEATRICE KYANDO
Mh.Beatrice Kyando akichangisha Mchango wa Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Jimbo Iwawa katiba Harambee iliyofanyika Usharika wa Ivalalila
Diwani
Viti maalumu Tarafa ya Lupalilo Mh.Beatrice Kyando kupitia Chama cha Demokrasia
na Maendeleo(CHADEMA) amewataka waumini wa Dini zote nchini kuwaombea Viongozi
wa nchi na Taifa kwa ujumla liendelee kuwa na Amani
Ameyasema
hayo mapema hapo jana akiwa katika Ibada ya kawaida na aliposhiriki Harambee
ya Ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Jimbo la Iwawa ambayo ilifanyika Usharika wa
Iwawa Wilayani Makete huku Sharika zingine ndani ya Jimbo la Iwawa zikifanya
Harambee kwenye sharika zao na Mh.Beatrice akishiriki Harambee hiyo na
Washarika wa Usharika wa Ivalalila
Mh.Beatrice Kyando amesema hakuna kazi nzuri inayofanywa bila Maombi kusikika kwa Mwenyezi Mungu
Hivyo waumini hawana budi kuliombea Taifa lao,Viongozi wa Serikali ngazi zote
ili waiongoze nchi kwa Hekima za Mwenyezi Mungu
"Jina la Bwana lihimidiwe washarika...sisi kama viongozi kwa ngazi tofautitofauti tunahitaji kuombewa maana pasipo maombi hakuna kiongozi ambaye ataongoza vizuri awe ni Rais,Waziri,Mkurugenzi au mkuu wa Wilaya na hata kitongoji kwa akili zake mwenyewe hawezi kuongoza la sivyo ataharibu kwa kila atakalolitenda,hivyo niwaombe viongozi hawa wanahitaji sana huduma yenu ya Maombi ili wazidi kufanya vizuri kwa Hekima na Busara za Mwenyezi Mungu"
Akiwa
katika Harambee hiyo Mh.Beatrice aliungana na washarika wa Usharika huo
kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Jimbo la Iwawa kwa kuchangia mchango wake wa kiasi cha shilingi Laki moja arobaini na mbili elfu(142,000)na washarika wakishiriki kwa upande wao kwa kuchangia shilingi elfu hamini na moja(51,000)katika ibada iliyoongozwa na Mchungaji Anjelika Sanga wa usharika huo
Mchungaji Anjelika Sanga akimshukuru Mh.Beatrice Kyando kwa Harambee na kukubali kushiriki kufanya ibada pamoja na waumini wa Usharika wa Ivalalila
Naye
Mtumishi wa Mungu aliyepata wasaa wa kuhubiri neno la Mungu kwa mara ya kwanza
kwenye Usharika huo wa Ivalalila Bw.Aldo Sanga ambaye pia ni Mwimbaji wa Nyimbo
za Injili amewataka waumini wa Kikristo kuwa na Matendo mema yenye kumpendeza
Mungu ili wasiomcha Mungu wasiwanyooshee Vidole kwa matendo yao mabaya
Ameongeza
kuwa Maisha ya kumcha Mungu yanachangamoto nyingi hivyo yanahitaji uvumilivu
katika kila linalotokea liwe baya au zuri
No comments