CHANJO YA MAJARIBIO YA EBOLA YAANZA KUTOLEWA LEO DRC
Shirika la afya Duniani (WHO) na Serikali ya Jamhuri ya Kidemkrasi ya Congo leo wameanzisha mpango wa kutoa chanjo ya majaribio dhidi ya ugonjwa wa Ebola ili kudhibiti kusambaa zaidi kwa virusi vya ugonjwa huo.
WHO linasema limewatambua zaidi ya watu 500 ambao huenda wamkaribiana na waathiriwa wa ugonjwa wa Ebola nchini Congo.
Huenda watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza leo watakaopewa chanjo hiyo ya majiribio.
- Ni kwanini Ebola inarudi mara kwa mara?
- Watoto na watu wazee ndio walichangia zaidi kusambaa kwa Ebola
Awamu ya kwanza ya chanjo hiyo ya majaribio iliwasili nchini Congo siku ya Jumatano.
Kumekuwa na milipuko mitatu ya Ebola nchini DRC tangu janga la mwaka 2014-2016 katika Afrika ya magharibi.
Dalili za Ebola
- Dalili za Ebola ni homa, kufuja damu na kuharibika kwa mfumo mkuu wa neva.
- Maafa ya ugonjwa huu huweza kufika asilimia tisini - lakini mzuko wa hivi punde unasababisha maafa 55% .
- Ugonjwa huo huchukua muda wa siku ishirini na moja kukomaa.
- Hakuna kinga wala tiba
- Huduma za msaada na kudhibiti kupoteza maji mwilini kutokana na kuharisha au kutapika husaidia katika kupona
- Inafikiriwa kuwa popo ndio hubeba virusi vya ugonjwa huo.
Ufanisi wa Chanjo ya Ebola
Uchunguzi uliofanyiwa chanjo ya ugonjwa wa Ebola mwaka jana umebaini kuwa inaweza kumkinga mtu kutokana na virusi vya ugonjwa huo kwa takriban mwaka mmoja.
Utafiti huo uliochapiswa katika jarida la New England Journal of Medicine, ulifanyiwa nchini Liberia na kuwashirikisha wagonjwa 1,500.
Wale waliopewa chanjo hiyo walifanikiwa kupata kinga yenye nguvu kwa karibu mwaka mmoja.
- WHO: Mlipuko wa Ebola DRC haujafika kiwango cha hali ya dharura
- Maisha baada ya janga la Ebola Afrika Magharibi
Majaribio hayo yanaonyesha kuwa chanjo hizo zote zinaweza kutumiwa kuokoa maisha wakati wa majanga ya ugonjwa wa Ebola siku za usoni.
Ugonjwa wa Ebola uliwaua zaidi ya watu 11,000 nchini Liberia, Sierra Leone na Guinea, wakati wa mlipuko wa ugonjwa huo mwaka 2014-2015.
No comments