WATENDAJI WA VIJIJI 50 KATI YA 53 WALIOACHISHWA KAZI WAREJESHWA KAZINI WILAYANI MAKETE
Watendaji 50 kati ya 53 wa vijiji
waliosimamishwa kazi kwa kukosa sifa za ufaulu wa kidato cha nne Wilayani Makete Mkoani Njombe
wameripoti Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Makete kwa
ajili ya kuendelea na kazi
Kufuatia agizo la waziri wa nchi ofisi ya Rais
Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora KAPTEN Mstaafu GEOGY MKUCHIKA utekelezaji
wake umeanza
Afisa Utumishi Wilaya ya Makete Bw.ASUKILE MBOGELA
Akizungumza na Kitulo Fm Mapema hii leo juu
ya kuripoti kwa Watendaji hao wa Vijiji Afisa Utumishi Wilaya
ya Makete Bw.ASUKILE MBOGELA amesema tayari Watendaji 50 wamesha ripoti katika
halmshauri ya Wilaya ya Makete Mkoani Njombe kwa ajili ya kuendelea na majukumu
yao huku watendaji wengine watatu wakiwa hawajaripoti kutokana na sababu
mbalimbali ikiwemo kustaafu,kugushi Cheti na mmoja kufariki dunia.
ASUKILE MBOGELA amewatoa hofu Watendaji hao
wa Vijiji juu ya mishahara yao ambayo hawajapata kwa kipindi chote ambacho
walisimamishwa kazi na amewataka kusubiri mara baada ya kujaza fomu maalumu kwa
kufuata taratibu watapatiwa Mishahara
hiyo.
Huku akiwataka watendaji hao ambao wanarejea
kazini kufanya kazi kwa weledi kwa kufuata kanuni na taratibu za utumishi wa
umma zinavyowataka
No comments