Header Ads

MDAU WA MAENDELEO MAKETE ATUNUKIWA CHETI MAALUMU NA BANK YA NMB NCHINI

Image may contain: 2 people, people standing, tree and outdoor
Kulia ni Ndg.Award Mpandila aliyetunukiwa cheti maalumu na Balozi wa Bank ya NMB Bw.Tomy kushoto ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Mikopo  

Katika shukrani zake kwa WanaMakete na Wadau wa Bank hiyo ya NMB nchini Bw.Award Mpandila katika Ukurasa wake wa Facebook amendika haya ''Siku ya leo(jana) namshukuru Mungu kwa baraka zake nimebahatika kutunukiwa cheti maalumu na bank bora nchini bank ya Nmb kama balozi wake.

Huduma za kibank ni muhimu saana kwa wateja na watanzania kwa ujumla,ongezeko na upanuzi wa huduma hizi hapa nchini umekuwa nimhimu kwa watanzania wote kwani kumekuwa na urahisi wa utoaji huduma mbali mbali
Watanzania sasa wanaweza kunufaika na huduma hizi pindi tu wanapoamua kujishugulisha na shughuli mbali mbali za kujiongezea kipato na kwa dhana hii ya watu kujihusisha na masuala ya kifedha (financial inclusion),katika maeneo mengi saana sasa mabenk yanafika na yanatoa huduma


Kifungu cha 71 cha sheria ya benki na taasisi ya kifedha ya mwaka 2000, 6 imetoa mwongozo mzuri wa namna ya kuendesha huduma kupitia mawakala ,ambapo hivi sasa benki yetu pendwa NMB wanamawakala karibia nchi nzima
Pia huduma zingine nyingi zinafanyika kirahisi zaidi kupitia matawi mbali mbali zaidi ya 600 na ATM zaidi ya 800 nchi nzima

Binafsi Nawapongeza saana uongozi na wafanyakazi wote nchi nzima wa bank ya NMB Benk nawapa heko saana kwa jinsi mnavyoendesha huduma za kibenk.nikiwa moja ya wateja wenu naahidi nitaendelea kuwa balozi mwema katika kufanikisha usambazaji wa huduma za kibenk kwa namna moja au nyingine"
Asante saana

No comments

Powered by Blogger.