MTOTO WA DARASA LA KWANZA ATWEKWA NA MWANAMKE WANGING'OMBE MKOANI NJOMBE
Kamanda Renatha Mzinga kulia
Jeshi la polisi Mkoa
wa Njombe linamshikilia Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la COLLETHA
NG'UMBI mkazi wa wilaya ya Wanging'ombe kwa kosa la kumteka mtoto mdogo
anayefahamika kwa jina la ERICK HOSEA MTEWELE mwanafunzi wa darasa la kwanza
wilayani hapo, na kuwataka wazazi wa mtoto huyo kutoa pesa ili waweze kurejeshewa
mtoto wao.
Akizungumza na waandishi wa habari kamishna msaidizi
mwandamizi wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe RENATHA MZINGA,amesema kuwa tukio la kutekwa kwa mwanafunzi huyo lilitokea
mnamo tarehe 11 mwezi wa 4 mwaka 2018 wilayani hapo wakati mwanafunzi akirudi
nyumbani.
Kamanda Mzinga amesema kuwa wakati shughuli za upelelezi
zikiendelea ili kumpata mtoto huyo, Baba mtoto aitwaye WILLIAM MTEWELE alianza
kupokea ujumbe mfupi uliomtaka mzee huyo aweze kutoa pesa kiasi cha shilingi laki
8 ili mtoto aweze kurejeshwa.
Aidha kamanda huyo wa polisi anasema kuwa jeshi la polisi
mara baada ya kuendelea kufanya upelelezi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo
akiwa na mtoto wake mwenye umri wa miaka miwili katika wilaya ya
mbarali mkoani Mbeya.
Katika hatua nyingine Kamanda mzinga amesema mara baada ya
kukamatwa kwa mwanamke huyo amedai kuwa alimchukua mtoto huyo na kutaka kiasi
hicho cha pesa ili aweze kulipa kiasi cha mahali alichokuwa akidaiwa na wazazi
wake na hivyo mpaka sasa jeshi la polisi linaendelea kumhoji mwanamke huyo.
No comments