MNYAMA KIBOKO ASHAMBULIA MASHAMBA NA KUHARIBU ZAO LA MPUNGA WILAYANI MAKETE
Zaidi ya Wakulima 15 Zao la Mpunga Kijiji cha Ruaha kilichopo Kata ya Mfumbi Wilayani
Makete Mkoani Njombe mashamba yao yameharibiwa vibaya na mnyama Kiboko.
Afisa Kilimo wa Kijiji cha Ruaha Kata ya Mfumbi Bw.HAMISI MKULICHE amesema wakulima 15 Mazao ya wakulima hao hasa zao la mpunga ambalo linalimwa kwa wingi
kijijini hapo yameharibiwa vibaya kufuatia uharibifu unaofanywa na mnyama huyo
Bwana HAMISI MKUCHIKA amewataka wakulima kuwa
wavumilivu kwani suala la kumtoa mnyama huyo katika mashamba hayo linafanyiwa kazi huku akiwataka wakulima kuwa makini wanapokwenda Mashambani mwao ili wasijeruhiwe na mnyama huyo
Wakulima wa Mpunga kijijini hapo wamesema Mnyama huyo amekuwa kishinda kwenye mashamba yao na kuharibu Mazao mbalimbali hususani Mpunga kwa zaidi ya wiki mbili sasa na kuziomba mamlaka husika kuchukua hatua za kumuondosha mnyama huyo kwenye mashamba yao
Naye Afisa Utalii Wilaya ya Makete Idara ya
Ardhi na Maliasili JOSHUA MUOGORO
amesema kwa eneo lolote ambalo linatukio la wanyama kuvamia mashamba ya
wakulima wanatakiwa kutoa taarifa kwa Mkurugenzi Mtedaji Wilaya ili Idara ya maliasili waweze kulishughulikia.
Bwana Joshua amewataka wananchi kutambua kuwa
tatizo kama hilo linapotokea hakuna fidia kwani eneo hilo ni mapito kwa wanyama
na amewataka wananchi kuchukua tahadhari kwani maliasili wameanza utaratibu wa kushughulikia
tatizo hilo
No comments