Header Ads

WADAU WA MAENDELEO MAKETE (MDA) WAJITOSA KUSAIDIA UJENZI WA BWENI LILILONGUA MANG'OTO SEKONDARI


KUTOKA DAWATI LA VIONGOZI CHAMA CHA MAENDELEO MAKETE (MDA)
No automatic alt text available.
Tumepokea kwa masikitiko taarifa ya kuungua bweni la Wanafunzi la shule ya Sekondari ya Mang'oto iliyopo kata ya Mang'oto Wilayani Makete, ambapo jengo liliungua pamoja na vitu mbalimbali vya wanafunzi yaani magodolo, vitanda, nguo, madaftari, vitabu, nk. Hasara inayotokana na moto huo inakadiriwa kufikia Milioni Mia Moja.
Chama cha Maendeleo Makete (MDA) inawapa pole wote walioguswa na janga hilo.
MDA kama mdau muhimu wa maendeleo wilayani Makete inaungana na wadau wengine kukusanya michango kwa ajili ya Shule ya Sekondari Mang'oto. 
Katika kufanikisha jambo hilo tunaomba makundi yote ya Makete pamoja na wadau wengine washirikiane katika kutoa michango mbalimbali kwa ajili ya Shule hiyo.
MDA itakusanya michango yote kupitia Makamu Mwenyekiti  wa umoja huo Philipo Mahenge kwa namba zifuatazo
MPESA0767902352
TIGOPESA0713902352
KUTOA NI MOYO
(Tutakusanya michango hadi tar 14.04.2018)
IMETOLEWA NA UONGOZI MDA
Kwa sasa wanafunzi wakiume wanajihifadhi kwenye vyumba vya Madarasa kufuatia kuungua kwa bweni lao

No comments

Powered by Blogger.