Header Ads

UNESCO YAWANOA MAFUNDI MITAMBO REDIO 25 ZA JAMII

 Afisa Miradi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) Rose Ngunangwa akifafanua jambo wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Mafundi Mitambo wa Redio za Jamii 25 yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) yaliyoanza tarehe 19 April 2018 na yanatarajiwa kukamilika tarehe 25 April 2018
 Baadhi ya Mafundi Mitambo wa Redio za Jamii wakiwa kwenye mafunzo ya Vitendo kwenye kituo cha TBC cha TAZARA wakati wa Mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa Redio za Jamii 25
Baadhi ya Mafundi Mitambo wa Redio za Jamii wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo mafundi mitambo wa Redio za Jamii 25

Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,Sayansi na Utamaduni(UNESCO) linatoa mafunzo ya siku saba kwa Mafundi mitambo 25 wa Redio Jamii kutoka Tanzania Bara na Zanzibar kwa lengo la kuwajengea uwezo kwenye utendaji wa kazi zao

Mafunzo hayo yanahusu masuala yanayoizunguka Jamii katika mahali ambapo Kituo cha Redio jamii kipo na namna ya kufanya mambo kitaalamu na kwa ufanisi ili kurusha Matangazo mazuri kwa wasikilizaji wake

UNESCO kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la Uswis(SDC) husaidia Redio za Jamii na Mtandao wa Redio hizo(TADIO)

Ufadhili huo unalenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania hususani waliopo Vijijini kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao kwa kupata taarifa ambazo ni sahihi kutoka kwa Redio hizo

Washiriki wanaofadhiliwa na(SDC) ni Kitulo Fm(Njombe),Nuru Fm(Iringa),Pambazuko Fm(Morogoro),Fadhila Fm(Mtwara),Jamii Mtu kwao(Mtwara),Loliondo Fm(Arusha),Baloha Fm(Shinyanga),Kahama Fm(Shinyanga),Ileje Fm(Songwe),Tripple A Fm(Arusha),Storm Fm(Geita)

Redio zingine ni Sengerema Fm(Mwanza),Kwireza Fm(Kagera),Dodoma Fm(Dodoma),Uvinza Fm(Kigoma),Mpanda Fm(Katavi),Pangani Fm(Tanga),Boma Fm(Kilimanjaro),Mazingira Fm(Mara),Mtegani Fm(Kusini Unguja),Mkoani Fm(Kusini Pemba),Micheweni Fm(Kaskazini Pemba),Tumbatu Fm(Kaskazini Unguja) na Ruangwa Fm(Lindi)



No comments

Powered by Blogger.