Header Ads

TUTAIHUBIRI INJILI POPOTE ULIMWENGUNI:-KWAYA YA NEEMA MAKETE MJINI



Mwenyekiti wa kwaya ya Neema Ndg.Fadhili Nkenza akizungumzia maandalizi ya Uzinduzi huo akiwa katika Studio za KituloFM Redio jana Jumapili kwenye kipindi cha Faraja yako

Kwaya ya Neema (KKKT-DKK) Makete Mjini inayofuraha kuwakaribisha wananchi wote katika uzinduzi wa DVD yao yenye jina lililobeba Album nzima ya “YESU MPONYA” mnamo tarehe 29 April 2018

Katika Uzinduzi huo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa ni Mwanamichezo maarufu nchini Ndg.Clement Sanga ambapo uzinduzi huo utafanyika Kanisa la KKKT Usharika wa Makete Mjini kuanzia saa 8:00 Mchana baada ya Ibada

Kwaya Mbalimbali zitakuwepo katika kusindikiza Uzinduzi huo ikiwemo kwaya ya Haleluya kutoka Iyunga Mbeya,Amkeni Kwaya kutoka Isapulano,Kwaya ya Wito kutoka Amani Bulongwa,Kwaya ya Kati Tandala,Mt.Cesilia Makete Mjini,Uvikanjo Makete Mjini,Kwaya ya Mwimbieni kutoka Bulongwa,Hosiana Kwaya kutoka Bulongwa,Kwaya ya Zaburi Idunda,Kwaya ya Ipelele na Waimbaji mbalimbali akiwepo Samsoni Kabiki,Aldo Sanga na wengine wengi watakuwepo

Mwenyekiti wa Kwaya hiyo Ndg.Fadhili Nkenza amesema kwaya hiyo imetoka mbali mpaka kufikia katika hatua ya uzinduzi huo pamoja na kukumbana na changamoto mbalimbali lakini walikuwa wakimtegemea Mungu wakati wote katika kazi hiyo

Nkenza amesema Uzinduzi wa Album hiyo ya DVD ni wa kwanza kufanyika kwa Kwaya hiyo tokea kuanzishwa kwake na malengo ni kuhubiri neno la Mungu kwa njia ya uimbaji popote ulimwenguni

Pia ameongeza kwamba wao kama kwaya wanajipanga kuwa na Website au Blog kwa ajili ya kusambaza kazi zao kupitia mitandao ya Kijamii ili kila mtu aweze kupata nyimbo zao kwa njia rahisi popote atakapokuwa

Angalia hapa chini picha za baadhi ya waimbaji wa kwaya hiyo wakiwa Studio za KituloFm Redio jana Jumapili





No comments

Powered by Blogger.