Header Ads

MWENYEKITI WA CHADEMA WILAYA YA MAKETE AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKIANA KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO BILA KUBAGUANA


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Makete Ndg.Ibrahim Ngogo amewataka wananchi wa kata ya Ikuwo na wanaMakete kwa Ujumla kushirikiana katika shughuli za Maendeleo bila kujali itikadi za Kisiasa katika kuiletea Maendeleo Wilaya ya Makete

Image result for ibrahim ngogo

Ndg.Ibrahim Ngogo Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Wilaya ya Makete

Ndg.Ibrahim Ngogo ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Wanachama wa Chama hicho kata ya Ikuwo kwenye mkutano wa ndani huku akiwasihi wananchi kwamba Siasa bila vitendo haziwezi kuleta Maendeleo hivyo wananchi wanatakiwa kushirikiana Pasipo kubaguana kwa itikadi za Vyama badala yake washiriki kikamilifu katika shughuli zote na Maendeleo

Wakati huohuo Ngogo amesema kama mtu atakataa kuchangia mchango wowote wa shughuli za Maedendelo kisa Itikadi za Kichama basi huyo haitakii mema Wilaya yake

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)Wilaya ya Makete Mh.Beatrice Kyando ameipongeza Serikali ya Awamu ya tano kwa uwajibikaji huku akisema ushirikano baina ya Viongozi uendelee ili kuleta Maendeleo

Image result for BEATRICE KYANDO

Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA)Wilaya ya Makete Mh.Beatrice Kyando 

Wakati huohuo amewataka wananchi wa kata ya Ikuwo kumuombea Diwani wa kata hiyo na kushirikiana naye katika shughuli za Maendeleo ili kufanikisha Malengo ya kuwatumikia wananchi wake waliomchagua

Katika Hatua nyingine Mh.Beatrice Kyando amewataka wanawake wa kata ya Ikuwo na kata zingine Wilayani Makete kuunda vikundi vya ujasiriamali vitakavyowasaidia kuinuana kiuchumi na siyo kubaki kuwa tegemezi kwa waume zao


No comments

Powered by Blogger.