Header Ads

DC MAKETE AZINDUA CHANJO MPYA YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI WILAYANI MAKETE

Elimu imetolewa kwa Taasisi za Umma na binafsi Wilayani Makete Mkoani Njombe kuhusu utolewaji wa Chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ‘Human Papilloma Virus Vaccine – HPV Vaccine' kwa ajili ya wasichana wenye umri wa miaka 14.

Wahudumu wa Afya ya Msingi,Walimu shule za Msingi na Sekondari kutoka maeneo mbalimbali ya Kata zote za Wilaya ya Makete wameanza kupata Elimu hiyo kwa ajili ya kusambaza kwa walengwa wanaokusudiwa kupatiwa huduma hiyo muhimu.

Zoezi la utoaji Elimu hiyo ya utolewaji wa Chanjo mpya ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi ‘Human Papilloma Virus Vaccine – HPV Vaccine' kwa ajili ya wasichana wenye umri wa miaka 14 imeanza kutolewa tokea mwishoni mwa wiki iiliyopita katika baadhi ya maeneo ya kata ya Ikuwo na sasa zoezi hilo linaendelea katika kata zingine 

Pia siku ya jana zoezi hilo limeendelea katika Kata ya Mfumbi,Matamba,Ikuwo,Lupila,Mbalatse,Ukwama,Mang'oto na Tandala

Hii leo zoezi hilo la utoaji wa Elimu hiyo linaendelea kata ya Kigulu,Bulongwa,Iwawa,Iniho na kata zingine zoezi litaendelea wiki hii

Uzizinduzi Rasmi wa Utoaji wa Huduma hiyo utafanyika kesho Kijiji cha Ivalalila kilichopo ndani ya Mamlaka ya Mji mdogo Iwawa na  baada ya hapo chanjo itaendelea kutolewa kwenye vituo vya kutolea huduma na katika shule.

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy akizungumza katika Uzinduzi wa Utoaji wa Huduma hiyo hapo jana katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Makete amebainisha kuwa walengwa wa chanjo hiyo ni wasichana wote waliotimiza miaka 14 ambapo wasichana 1,397 wanatarajiwa kuchanjwa ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani ya mlango wa kizazi katika Wilaya ya Makete.

ANA MARIA KANYAWANI ni Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Wilaya ya Makete amezitaja baadhi ya sababu zinazosababisha Saratani ya Mlango wa Kizazi kuwa ni Uvutaji wa Sigara,Kuanza kujamiiana  katika na umri Mdogo,kuoa Mitara pamoja na kuwa na wapenzi wengi.

Mganga Mkuu Wilaya ya Makete Daktari ITIKIJA MSUYA amesema huduma ya Chanjo ya  Saratani ya  Mlango wa Kizazi imeshaanza baadhi ya maeneo  ikiwemo Kijiji cha Ikuwo Kata ya Ikuwo lakini itazinduliwa rasmi tarehe 25 mwezi 4 mwaka huu  katika Kata ya Iwawa Kijiji cha Ivalalila.

Kwa Mujibu wa Shirika la Afya Duniani [WHO] inakadiliwa kuwa kila Mwaka ni Kati ya Wanawake laki nne na sitini na sita (466,000) wamebainika kuwa na Saratani  ya Mlango wa Kizazi na wengi wao wako katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania.
 Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Makete Mh.Veronica Kessy,kushoto kwake ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Makete Mh.Jison Mbalizi,kushoto kwake pia ni Afisa Utumishi Wilaya Bi.Rosemary Iresa,wa kwanza kutoka kushoto ni Mganga Mkuu Wilaya Daktari Itikija Msuya,anayefuata ni Grecy Mgeni Katibu Tawala Wilaya ya Makete
Baadhi ya wadau kutoka Taasisi Mbalimbali,Idara mbalimbali na Vingozi wa Dini walioshiriki katika Ufunguzi wa Huduma hiyo

No comments

Powered by Blogger.