WALIMU 77 SHULE ZA SEKONDARI WAPELEKWA SHULE ZA MSINGI WILAYANI MAKETE
Walimu 77 wamehamishiwa shule mbalimbali za Msingi kutoka shule za Sekondari Wilayani Makete Mkoani Njombe
Akizungumza na Morning Power hapa Kitulo RedioFm Afisa Elimu Msingi Wilaya ya Makete Mwl.Antony Mpiluka amesema walimu hao wamepelekwa shule za Msingi kusaidia kuinua kiwango cha Taaluma Elimu ya Msingi
Mpiluka ameongeza kwamba kutokana na tatizo la upungufu wa Ikama kati ya walimu na wanafunzi kumekuwapo na changamoto kubwa ya walimu kuzidiwa na mzigo mkubwa wa kufundisha sababu inayopelekea kiwango cha taaluma kushindwa kufikia malengo katika ufaulu wa juu zaidi
Wakati huohuo ameeleza kuwa baadhi ya walimu hawajaripoti kwenye vituo vyao vipya vya kazi mpaka sasa hivyo amewataka kuripoti kwenye vituo vyao vya kazi haraka iwezekanavyo,kwa kuwa ambaye hatofanya hivyo hatua za kiutumishi zitafuatwa dhidi yake
Vilevile amewataka wazazi kutoa ushirikiano mkubwa kwa walimu hao ili kuwatia moyo wa kufanya kazi kwenye Mazingira yanayovutia na siyo kuwatenga walimu hao wasije wakaanza kujisikia vibaya na kujiona kama wametengwa
No comments