Header Ads

SHIRIKA LA MAPAO WILAYANI MAKETE KUWA MFANO WA KUIGWA KWA KUISAIDIA JAMII

 Kutoka kushoto ni Wananchi wa kata ya Tandala wakimuelekeza M/kiti wa Bodi ya Mapao Wilaya ya Makete Ndg.Falmeo Mahenge(Kulia) wanavyosaidiwa mambo mbalimbali yanayohusu usaidizi wa kisheria
 Joseph Shabani Magazi Afisa Mradi kutoka LSF Zanzibar kutoka kushoto akizungumza na Baadhi ya watumishi wa Umma katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makete
 Simon Henry kutoka Makao Makuu ya LSF Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimba wa ufuatialiaji kutoka ngazi ya Mkoa wa Njombe akizungumza kuhusu Wasaidizi wa kisheria namna wanavyofanya kazi ya kuwasaidia wananchi katika kutatua migogoro na kupata haki akiwa ofisi ya Mkuu wa Wilaya Makete
 Wageni hao walitembelea pia ofisi za Kitulofm Redio ambayo inafanya vipindi mbalimbali na wasaidizi wa Kisheria Wilayani hapa kila wiki mara moja
Timu ya ufuatiliaji Ngazi ya Taifa kutoka Shirika la  LSF Wasaidizi wa Kisheria wametembelea na kuona Shughuli zinazofanywa na wasaidizi wa kisheria ngazi ya Wilaya na kata Wilayani Makete Mkoani Njombe huku ikipongeza kazi kubwa inayofanywa na wasaidizi hao na kuongeza kwamba inafaa kuwa mfano wa Kuigwa na wasaidizi hao Wilaya zingine

Pongezi hizo zimetolewa na Ndugu Joseph Shabani Magazi Afisa Mradi kutoka LSF Zanzibar akiwa Wilayani hapa akiongozana na Simon Henry kutoka Makao makuu ya LSF Dar es salaam pamoja na viongozi mbalimba wa ufuatialiaji kutoka ngazi ya Mkoa wa Njombe

Vincent Msigwa mkaazi wa kijiji cha Ikonda kata ya Tandala amesema uwepo wa MAPAO umewafanya wananchi kujua mengi kuhusu migogoro na namna ya kutatuliwa kwa kuwa yeye ni miongoni mwa waliosaidiwa na MAPAO

Akitolea ushuhuda ameongeza kuwa alikuwa na mgogoro na jirani yake ambapo Mifugo yake(Ng'ombe) ilikula mahindi ya jirani kilo tano na alishtakiwa kwa Mtendaji wa kijiji na akaambiwa alipie Milioni mbili lakini baada ya kukutana na Msaidizi wa kisheria kata ya Tandala Bw.Naumu Sanga na kuwaeleza shida hiyo waliitatua kwa kulipa mahindi lita tano tu badala ya fedha talimu Milioni mbili


Mkurugenzi wa Wasaidizi wa Kisheria Wilayani Makete Mch.Denis Sinene amesema Shirika la MAPAO kwa sasa limekuwa likifanya kazi kwa ufanisi mkubwa kutokana na mafanikio wanayoyapata kwa kutatua changamoto na migogoro mingi inayoikumba jamii hususani kwenye migogoro ya ndoa,Ardhi na mirathi

No comments

Powered by Blogger.