MIMBA ZA UTOTONI KAZI KWA WAZAZI
Wito umetolewa kwa wazazi wa watoto wa kike wanaokatishwa masomo yao kwa kupata mimba kuwachukulia hatua za kisheria wale wote wanaohusika na kuwapa mimba watoto wao ili kukabiliana na tatizo la mimba za utotoni.
Hayo yameelezwa na Ofisa Ustawi wa jamii wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma, Anthony Mbabile wakati wa Mafunzo yanayohusu ulinzi kwa mtoto wa kike ili kumkinga na mimba za utotoni yaliyotolewa na shirika lisilo la kiserikali la Jukwaa la utu wa Mtoto (CDF).
Mbabile amesema kuwa tatizo la mimba za utotoni Wilayani Mpwapwa ni kubwa kwa kuwa wazazi wa watoto wa kike wanaopewa mimba hawataki kuwaripoti wale waliowapa mimba watoto wao na hivyo kulazimika kumalizana nje ya vyombo vya sheria.
Naye Ofisa ustawi wa Jamii wa Kata ya Pwaga katika halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, Patrick Mafuru amesema kuwa elimu ya afya ya uzazi ni muhimu kutolewa kwa vijana pamoja na wadau wa mtoto ili waweze kujua madhara yanayoweza kuwapata kwa kubeba mimba kabla ya kufikisha umri unaotakiwa.
No comments