WANAUME MAKETE WASHAULIWA KUSHIRIKI UZAZI WAMPANGO
Wito umetolewa kwa wanaume
wilayani makete mkoani njombe kutambua umuhumi wa kushiriki katika uzazi wa mpango ili kuleta
maendeleo hapa nchini
Akizungumza na Kitulo Fm
muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Makete
Bi.Anna Mbilinyi amesema umuhimu
wa wanaume kushiriki katika uzazi wa Mpango husaidia kuinua uchumi na kuleta
maendeleo katika Famili na Taifa kwa ujumla
Bi.Anna Mbilinyi
amesema Wilaya ya Makete wanaume wamekuwa
na mwitikio mdogo na ni wanaume wachache
wanao kubaliana na suala hilo
Pia amesema uzazi wa mpango unaweza kumkinga
mtu na mangojwa mbalimbali ya kuambukizwa kama Virusi vya Ukimwi,Kaswende na
magonjwa mengine mbalimbali.
No comments