Elimu ya hedhi salama imetolewa kwa shule za seKondari na msingi wilayani Makete
Shirika lisilo la kiserikali
linalojihushisha na utoaji elimu ya uzazi mashuleni (SAWA) kwa kushirikiana na
kitulo fm radio limetoa rai kwa Wazazi
na walezi wa watoto wa kike wilayani makete mkoani njombe kuwapa elimu watoto
wao pindi wanapo pata hedhi.
Rai hiyo imetowa na Bi Monika mahenge ambaye ni mratibu wa afya mashuleni
wakati wa utoaji elimu ya uzazi katika
shule ya sekondari kitulo iliyopo wilayani makete mkoani njombe mapema wiki hii
ambapo ammesema kuwa kuna baadhi ya
watoto wa kike ambao hawajapata elimu juu ya mtumizi sahii ya peds pindi wawapo
kwenye hedhi ambapo wanatumia vitu visivyo salama katika kujikinga kwa kutumia
manyoya ya kuku ,mavi ya ng'ombe na mchanga kitu kinachohatarisha maisha yao.
Aidha bi mahenge ameongeza
kuwa pindi mtoto wa kike au wakiume
awapo kwenye kipindi cha ukuaji anapaswa kuwa msafi kwa kujinyoa nywele zinazoota sehemu za siri.
pia Bi Monika ametoa elimu
kwa mtoto wa kike anapokuwa kwenye hedhi anapaswa kujisafisha vizuri sehemu za
siri ili zisitoe harufu na kuvaa nguo za ndani safi na kavu pamoja na utupaji
wa pedi salama
No comments