Rais Mstaafu Kikwete atuma salamu kwa hili lililomgusa leo
Rais
mstaafu wa serikali ya awamu ya nne ya Jamhrui ya Muungano wa Tanzania
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ameipongeza timu ya taifa ya Zanzibar
(Zanzibar Heroes) baada ya kutinga fainali ya CECAFA 2017
Zanzibar
Heroes imetinga fainali baada ya kumfunga 2-1 bingwa mtetezi wa
michuano hiyo Uganda kwenye mchezo wa nusu fainali ya CECAFA Senior
Challenge uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa Moi mjini Kisumu
Kenya.
“Nawapongeza
Zanzibar Heroes kwa kututoa kimasomaso na kutinga fainali. Nawatakia
kila la kheri katika mechi ya fainali waibuke na kombe na watupe raha
ambayo Watanzania tumeikosa kwa muda mrefu”, ameandika Dkt. Kikwete
kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.
Rais
huyo mstaafu anasifika kwa kupenda michezo na akiwa madarakani amewahi
kumlipa mshahara aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ‘Taifa Stars’ kwa
wakati huo Marcio Maximo.
Zanzibar
Heroes itacheza mchezo wa fainali siku ya Jumapili dhidi ya wenyeji
Kenya. Katika michuano hiyo Tanzania iliwakilishwa na timu ya
Kilimanjaro Stars ambayo haikufanya vizuri baada ya kuondolewa katika
hatua ya makundi ikiwa na alama moja tu.
No comments